LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAGANGA WA KIENYEJI 55 MBARONI KWA TUHUMA ZA UPIGAJI RAMLI. PIA WAKUTWA NA NYWELE ZA ALBINO.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Valentino Mlowola (katikati) akiwaonyesha wanahabari (hawapo pichani) nywele zinazosadikiwa kuwa za mtu mwenye ulemavu wa ngozi ikiwa ni miongoni mwa vitu walivyokamatwa navyo watuhumiwa wa shughuli za upigaji ramli Mkoani Mwanza.
Na:Gerge Ninagi-GB Pazzo
Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza limewatia nguvuni watu 55 wanaosadikiwa kuwa Waganga wa Kienyeji kwa tuhuma za kujihusisha na shughuli za Upigaji wa haramu chonganishi, ambao umepelekea kushamiri kwa mauaji ya watu wenye Ulemavu wa ngozi pamoja na Vikongwe hapa nchini.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Valentino Mlowola aliyasema hayo jana, wakati akizungumza na Wanahabari Ofisini kwake kuhusiana na Kukamatwa kwa Watu hao ikiwa ni matokeo ya Oparesheni iliyoanza tangu tarehe sita mwezi huu katika Wilaya zote za Mkoa wa Mwanza ikiwa imelenga Kuwasaka Waganga wote wa Kienyeshi wasio na Vibari sanjari na wanaopiga ramli chonganishi.

Kamanda Mlowola alibainisha kuwa miongoni mwa watuhumiwa waliokamatwa katika Oparesheni hiyo, wanawake ni 18 na wanaume ni 37 ambapo watuhumiwa hao pia wamekutwa na nyara za Serikali ambazo ni pamoja na ngozi za Fizi, Mbweha, Digidigi, Simba, Kenge, Chui, Nungunungu na Chatu Chatu pamoja na mikia na pembe za wanyama pori mbalimbali.

Alisema kuwa Watu hao wamekamatwa na Vifaa mbalimbali walivyokuwa wakivitumia kwa ajili ya shughuli za kupigia ramli ambavyo ni pamoja na Simbi, Vibuyu, Ungo, Visonzo, Kigoda, ngoma, shanga, manyanga, njuga, nywele zinazoaminika kuwa za mtu mwenye ulemavu wa ngozi pamoja na fedha ambazo ni noti na sarafu za zamani.

Aliongeza kuwa tayari baadhi ya Watuhumiwa wamefikishwa mahakamani huku wengine wakiendelea Kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya Upelelezi ambapo watafikishwa Mahakamani pindi upelelezi Utakapo Kamilika.

Aidha Kamanda Mlowola alisema kuwa Msako huo ni endelevu na ametoa rai kwa waganga wote wa kienyeji wanaojihusisha na Vitendo vya Kupiga ramli kujisalimisha mara moja wakiwa na nyenzo zao kwa kuwa vitendo hivyo vinaipotosha jamii ikiwa ni pamoja na wananchi kuaminishwa kwamba viungo vya watu wenye ulemavu wa ngozi vinasaidia kuleta utajili hali ambayo imekuwa ikiongeza vitendo vya Ukatili na Mauaji kwa watu hao.

Mbali na hayo, Kamanda Mlowola alibainisha kuwa jeshi la Polisi Mkoani Mwanza halijalala hivyo juhudi za kumtafuta mtoto mwenye ulemavu wa ngozi Pendo Emmanuel (4) alietekwa na Watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwao Wilayani Kwimba Mwishoni Mwa Mwaka jana bado zinaendelea ambapo amebainisha kuwa watu kadhaa wanashikiriwa kwa ajili ya mahojiano zaidi lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa mtoto huyo anapatikana aidha akiwa hai ama la.

Katika hatua nyingine Kamanda Mlowola alibainisha kwamba, Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza limefanikiwa kuwakamata Watu Sita raia wa Ethiopia, kwa kosa la kuingia hapa nchini kinyume cha Sheria.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Valentino Mlowola (katikati) akiwaonyesha wanahabari (hawapo pichani) baadhi ya nyara mbalimbali za serikali walizokamatwa nazo watuhumiwa wa shughuli za upigaji ramli Mkoani Mwanza.
Hii ni ngozi ya Simba ikiwa ni miongoni mwa nyara walizokamatwa nazo watuhumiwa wa shughuli za Upigaji Ramli Mkoani Mwanza.
Baadhi ya Vitendea Kazi walivyokamatwa navyo Waganga wa Kienyeji wanaotuhumiwa kujihusisha na Shughuli za Upigaji Ramli Mkoani Mwanza.
Hizi ni baadhi ya Ngozi ambazo walikamatwa nazo waganga wa Kienyeji Mkoani Mwanza Kwa tuhuma za Kujihusisha na Shughuli ya Upigaji ramli ambayo imepigwa marufuku na Serikali.
Hii ni ngozi ya Kenge ambayo walikamatwa nayo waganga wa Kienyeji Mkoani Mwanza ambao wanatuhumiwa Kujihusisha na Shughuli ya Upigaji ramli ambayo imepigwa marufuku na Serikali.
Fuvu la kiumbe ambacho bado hakijafahamika pamoja na nywele zinazosadikika kuwa za mtu mwenye ulemavu wa ngozi ni miongoni mwa vitu walivyokamatwa navyo watuhumiwa wa shughuli ya upigaji ramli Mkoani Mwanza.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Valentino Mlowola.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Valentino Mlowola (katikati) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) ofisini kwake jana jijini Mwanza.
Wanahabari

No comments:

Powered by Blogger.