LIVE STREAM ADS

Header Ads

WANANCHI WAVUNJA UKUTA ULIOKUWA UMEJENGWA ENEO LA MSIKITI WA WAARABU MAKOROBOI.

Huu ni Ukuta uliovunjwa jana na kundi la watu waliokuwa wakijiita Wananchi katika eneo la Makorobi karibu na Msikiti wa Tample Maarufu kwa jina la Msikiti wa Waarabu. Baada jeshi la Polisi kikosi cha kutuliza ghasia kiliweza kulitawanya kundi hilo ambalo lilieleza kuwa halihusiana kwa namna yoyote ile na kundi Wamachinga Jijini Mwanza.
Na: George Binagi-GB Pazzo
Kundi kubwa la Wananchi Jijini Mwanza limeng'oa nguzo zilizokuwa zimewekwa katika barabara ya inayoingia katika eneo la Makoroboi karibu na Msikiti wa Temple Maarufu kama Msikiti wa Waarabu ikiwa ni pamoja na kuvunja ukuta uliokuwa umejengwa katika eneo hilo.

Wananchi hao walifikia hatua hiyo juzi ijumaa baada ya kudai kuwa barabara hiyo inapaswa kuwa wazi na haipaswi kufungwa kwa namna yoyote ile, kwa kuwa barabara hiyo hutumiwa na baadhi ya wafanyabiashara kuingiza bidhaa zao katika maduka yaliyo katika eneo la Makoroboi sanjari na kutumiwa wazazi wazaowapeleka watoto wao wanaosoma shule ya awali ya Rajendra iliyopo karibu na Msikiti huo wa Temple (Msikiti wa Waarabu).

Walieleza kuwa awali ukuta huo uliokuwa umejengwa katika eneo hilo la barabara ya Temple iliamuliwa na Baraka Konisaga ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana kuwa ubomolewe lakini utekelezaji haukuweza kufanyika, kabla ya jana tena kukuta nguzo zimewekwa katika barabara inayoingia katika eneo hilo na ndipo wakafikia maamuzi ya kuzing'oa sanjari na kubomoa ukuta huo wao wenyewe.

Hatimae wananchi hao walifanikiwa kuvunja Ukuta huo uliokuwa umejengwa katika eneo hilo la Temple ( Msikiti wa Waarabu sanjari na kung'oa nguzo hizo ambazo ni za zege zilizokuwa zimesimikwa katika barabara ya kuingia katika eneo hilo, kabla ya Jeshi la polisi Mkoani Mwanza kupitia kikosi cha kuzuia ghasia kuwatawanya kwa kutumia mabomu ya kutoa machozi.

Kingo na Kuta hizo zilielezwa kujengwa na Uongozi wa Msikiti wa Temple (Msikiti wa Waarabu) kwa lengo la kuzuia muingiliano wa aina yoyote katika eneo hilo.

Hata hivyo wananchi hao walisisitiza kuwa kilichofanyika jana kisihusishwe kwa namna yoyote ile na Kundi la Machinga Jijini Mwanza, kwa kuwa uamuzi wa kuvunja Ukuta huo sanjari na kung'oa nguzo hizo ni uamuzi wa Wananchi Jijini Mwanza na siyo uamuzi wa Machinga.

Hakuna mwandishi wala mtu yeyote alieruhusiwa kupiga picha katika eneo hilo hali iliyopelekea baadhi ya watu kupokea kichapo pale walipoonekana kupiga picha kwa kutumia simu zao ambapo hata hivyo baadae kabisa Binagi Media Group iliporuhusiwa kupiga picha kwa masharti ya kutojumuisha picha za Umati wa watu waliokuwa katika eneo hilo. 

"Mwanzo hali ilikuwa ngumu kwani nusra nipigwe na Kunyang'anywa Kamera niliyokuwa nayo baada ya kufika katika eneo la tukio na kamera yangu kwa ajili ya kazi ambapo mzozo ulitokea kwa sekunde kadhaa lakini baadhi ya wananchi waliingilia kati na kuniruhusu kufanya kazi yangu kwa masharti ya kutopiga picha zinazoonyesha Ummati wa wananchi hao".

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mwanza, Valentino Mlowola alisema wanawashikilia vijana 12 waliokuwa wanahusika katika tukio hilo.
Tulichofanya tumedhibiti hali ya fujo iliyokuwa imeanza kujitokeza na sasa tunachunguza iwapo ujenzi huo ulikuwa na kibali,” alisema Kamanda Mlowola.
Huu Ukuta nao ulikuwa umeanza kuvunjwa na Wananchi katika eneo la Makorobi karibu na Msikiti wa Tample Maarufu kwa jina la Msikiti wa Waarabu. Hata hivyo jeshi la Polisi Mkoani Mwanza kupitia kikosi cha kutuliza ghasia liliweza kulitawanya kundi hilo ambalo lilieleza kuwa halihusiana kwa namna yoyote ile na kundi Wamachinga Jijini Mwanza.
Hili ndilo eneo lililovunjwa na Kundi kubwa la Wananchi Jijini Mwanza kwa kile walichodai kupiga Uwepo wa Ukuta huu katika eneo la Makoroboi Karibu na eneo la Msikiti wa Temple Maarufu kama Msikiti wa Waarabu. Upande wa Kusho kama unavyoonekana tayari ulikuwa umevunjwa kabla kundi hilo kutawanyishwa na jeshi la Polisi Mkoani Mwanza kupitia kikosi cha kuzuia hasia kwa kutumia mabomu ya kutoa machozi.
Hapa ndipo kulikuwa na Nguzo za Zege zilizokuwa zimechimbiwa chini kwa lengo la kuzuia Magari kuingia Makoroboi karibu na Msikiti wa Temple maarufu Kama Msikiti wa Waarabu. Binagi Media Group haikufanikiwa kupata picha za nguzo hizo baada ya kuzuiliwa na kundi la Wananchi waliokuwa wakizing'oa nguzo hizo.

2 comments:

  1. mmmhhh ! ile si ni njia ya kijamii !!

    ReplyDelete
  2. mmmmmmhhh!! ile si ni njia na barabara ya kijamii !!!

    ReplyDelete

Powered by Blogger.