 |
Baadhi ya Waganga na Wakunga (Wataalamu) wa Tiba Asilia wakiwa katika Kikao chao cha Kulaani Mauaji ya Albino pamoja na wao Kuhusishwa katika Mauaji hayo kilichofanyika jana maeneo ya Nera Wilayani Ilemela zilipo Ofisi za Chama cha Waganga na Wakunga wa Tiba Asilia Tanzania CHAWATIATA. |
Na: George Binagi-GB Pazzo
Chama
cha Waganga na Wakunga wa Tiba Asilia Tanzania CHAWATIATA Mkoa wa Mwanza,
kimeandaa Maandamano ya Amani kwa ajili ya Kulaani Vitendo vya Utekwaji na
Mauaji ya Watu wenye Ulemavu wa ngozi hapa nchini.
Uongozi wa Chama hicho ulitoa kauli hiyo jana Mkoani Mwanza,
katika kikao cha pamoja na Wanachama wa CHAWATIATA Mkoa wa Mwanza, kilichokuwa
kimelenga kulaani Mauaji ya Albino hapa nchini, sanjari na kulaani Wanganga na
Wakunga wote wa Tiba asilia kuhusishwa katika Mauaji hayo hali ambayo
imepelekea kusakwa na kukamatwa na Jeshi la Polisi katika Maeneo mbalimbali
hapa nchini.
Maandamano
hayo yanatarajiwa kufanyika March 28 mwaka huu ambapo Kawawa Athuman ambae ni Katibu wa CHAWATIATA Mkoa wa Mwanza
alisema kuwa Chama Kimeandaa Maandamo hayo ya Amani kwa ajili ya Kupinga Mauaji
ya Albino ambayo yatatoa fursa kwa Waganga na Wakunga wa Tiba Asilia kutoa kauli
zao kuhusiana na Mauaji hayo.
Nae Hamis Hassan ambae ni Mwenyekiti wa CHAWATIATA Mkoa wa Mwanza
alisema kuwa Chama kinalaani vikali ramli Chonganishi, Mauaji ya Albino pamoja na
Vikongwe huku akiongeza kuwa Chama kinapinga Waganga na Wakunga wote kuhusishwa
katika mauaji ya Albino na Vikongwe hapa nchini.
Alisema kuwa katika tiba asilia hakuna kiungo cha Albino kinachoonekana
tiba hivyo yeyote anaeshiriki kuchukua kiungo chochote cha Albino achukuliwe
kama muuaji na si mganga na ahukumiwe kisheria na si kuwahukumu waganga wote
kama ambavyo jeshi la pilisi limekuwa likiwakamata waganga wote kwa tuhuma za
kujihusisha na Mauaji ya Albino hapa nchini.
Nao baadhi ya Waganga na Wakunga wa Tiba Asilia ambao ni Wanachama
wa CHAWATIATA walieleza kuwa wao hawahusiki na Mauaji ya Albino na Vikongwe hapa
nchini huku wakiongeza kuwa kitendo cha Polisi kukamata vifaa vyao vya Uganga
si sahihi hivyo hali hiyo inaashiria yaliyoandikwa kuwa mila na desturi za
Mwafrika zitakwisha na utamaduni wa mwafrika utakufa ndiyo yameanza kutimia.
Wengine waliongeza kuwa kuna baadhi ya watu wachache wanaoharibu sifa
za Waganga wa Tiba Asilia hivyo Serikali kupitia jeshi la polisi kuwabaini watu
hao, badala ya kuwakamatwa waganga na wakungwa wote wa Tiba Asilia kwa tuhuma
za kujihusisha na Mauaji ya Albino na Vikongwe hapa nchini jambo ambalo
linaleta uchonganishi kati ya Waganga na Albino wakati kuna baadhi ya Waganga
wamezaa Albino na kuwalea vyema.
Hayo yamejili siku chache baada ya Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza
kupitia kwa Kamanda wake Valentino Mlowola kueleza kuwakamata Waganga wa
Kienyeji wapatao 55 wasiokuwa na vibali vya kufanya shughuli hiyo, kwa tuhuma
za kujihusisha na Shughuli za upigaji wa Ramli chonganishi hali ambayo imekuwa
ikisababisha uchonganishi katika jamii sanjari na kuchochea Mauaji ya Albino na
vikongwe hapa nchini.
 |
Baadhi ya Waganga na Wakunga (Wataalamu) wa Tiba Asilia wakiwa katika Kikao chao cha Kulaani Mauaji ya Albino pamoja na wao Kuhusishwa katika Mauaji hayo. |
 |
Baadhi ya Wataalamu wa Tiba Asilia wakiwa katika Kikao chao cha Kulaani Mauaji ya Albino pamoja na wao Kuhusishwa katika Mauaji hayo. |
 |
Baadhi ya Viongozi wa CHAWATIATA Mkoa wa Mwanza wakiwa katika Kikao chao cha Kulaani Mauaji ya Albino pamoja na wao Kuhusishwa katika Mauaji hayo. |
 |
Wataalamu wa Tiba Asilia wakiwa katika Kikao chao cha Kulaani Mauaji ya Albino pamoja na wao Kuhusishwa katika Mauaji hayo. |
 |
Aliesimama ni Hamis
Hassan ambae ni Mwenyekiti wa CHAWATIATA Mkoa wa Mwanza. |
 |
Kawawa
Athuman (Aliesimama) ambae ni Katibu wa CHAWATIATA Mkoa wa Mwanza. |
 |
Aliesimama ni Mmoja wa wataalamu wa Tiba asili akizungumza kulaani Mauaji ya Albino hapa nchini ikiwa ni pamoja na Waganga na Wakunga wa Tiba Asilia kuhusishwa katika Mauji hayo. |
 |
Miongoni mwa wataalamu wa Tiba asili akizungumza kulaani Mauaji ya Albino hapa nchini ikiwa ni pamoja na Waganga na Wakunga wa Tiba Asilia kuhusishwa katika Mauji hayo. |
 |
Mmoja wa wataalamu wa Tiba asili akizungumza kulaani Mauaji ya Albino hapa nchini ikiwa ni pamoja na Waganga na Wakunga wa Tiba Asilia kuhusishwa katika Mauji hayo. |
 |
Mmoja wa wataalamu wa Tiba asili akizungumza kulaani Mauaji ya Albino hapa nchini ikiwa ni pamoja na Waganga na Wakunga wa Tiba Asilia kuhusishwa katika Mauji hayo. |
 |
Mtaalamu wa Tiba asili akizungumza kulaani Mauaji ya Albino hapa nchini ikiwa ni pamoja na Waganga na Wakunga wa Tiba Asilia kuhusishwa katika Mauji hayo. |
No comments: