LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWILI WA MAREHEMU MARSH KUWASILI JIJINI MWANZA. WADAU WATETA MWILI WAKE KUSAFIRISHWA KWA GARI.

Asha Sylivester Marsh (Wa Pili Kushoto) ambae ni Mjane wa aliekuwa Kocha Msaidizi wa Timu ya Soka ya Taifa na aliewahi pia kuwa Kocha wa Klabu mbalimbali za Soka hapa nchini Marehemu Sylivesta Marsh akiwa na ndugu wengine wakiwa Msibani Kwa Marehemu Mirongo Jijini Mwanza wakiusubiri mwili wa Marehemu ambao unatarajiwa kuwasili hii leo jioni kutoka Jijini Dar es Salaam.
Marehemu Marsh alizaliwa mwaka 1960 na alifariki juzi Jumamosi March 14 majira ya Alfajili akiwa katika Hospital ya Taifa Mhimbili kwa ajili ya Matibabu ambapo inaelezwa kuwa alianza kusumbuliwa na maradhi takribani mwaka mmoja uliopita.
Na:George Binagi-GB Pazzo
Badrudini Nsubuga (Mwenye daftari) ambae ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi ya Marehemu Kosha Marsh akiwa pamoja na Jumanne Shengelo ambae ni Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Mkoani Mwanza MZFA (Wa kwanza Kushoto) pamoja na viongozi na wadau wengine wa Michezo nyumbani kwa marehemu Mirongo Jijini Mwanza kwa ajili ya Maandalizi ya Kuupokea Mwili wa Marehemu kutoka Jijini Dar es salaam hii leo Alasiri.
Badrudini Nsubuga (wa tatu pande zote) ambae ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi ya Marehemu Kosha Marsh akitoa ratiba kamili ya Msiba wa Marehemu Marsh wakati akizungumza na Metro Fm & Binagi Media Group.
Wakizungumza kwa masikitiko Makubwa baadhi ya wadau wa michezo Jijini Mwanza wameeleza kusikitishwa kwa kitendo cha mwili wa Marehemu Mwalimu Marsh kusafirishwa kwa njia ya barabara (Kwa gari/ Coaster) kutoka Jijini Dar es salaam hadi Jijini Mwanza ukilinganisha nafasi aliyokuwa nayo katika Soka la Tanzania.

Wameongeza kuwa wamesikitishwa namna Chama cha Soka Mkoani Mwanza MZFA pamoja na Shirikisho la Soka nchini TFF walivyoshindwa kumuenzi Marehemu Mwalimu Marsh hususani kwa namna mwili wake ulivyosafirishwa sanjari na katika michezo ya ligi kuu ya Tanzania bara iliyochezwa jana kushindwa kuonyesha ishara ya aina yoyote ya kumuenzi marehemu Marsh.
BINAGI MEDIA GROUP: PUMZIKA KWA AMANI KOCHA MZALENDO MARSH.

1 comment:

  1. tumesikitika kuondokewa na mtaalam huyu wa soka......lakini pia ni muhimu wadau wote wa soka hasa wachezaji kuandaa maisha yao ya baadaye ili kuondokana na utegemezi wa misaada wakati wa matatizo ya kuugua na misiba...

    ReplyDelete

Powered by Blogger.