LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKUTANO WA HADHARA WA KATIBU WA CCM MKOANI MWANZA WAACHA HISTORIA JIJINI MWANZA.

Umati wa Wananchi na Wakereketwa wa Chama cha Mapinduzi CCM wakiwa katika Mkutano wa hadhara wa Chama hicho uliofanyika jana Igoma Stand Jijini Mwanza ambapo Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu alikuwa akihutubia katika Mkutano huo.
Mkutano huo ulikuwa ni Sehemu ya ziara ya Mtaturu katika Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza ambapo kabla ya Mkutano huo alipata fursa ya kutembelea miradi mbalimbali ya Maendeleo katika Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza ili kujionea Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010/15.

Ziara ya Mtaturu ilianza March 22 mwaka huu katika Wilaya ya Ukerewe na Kufuatiwa na Wilaya za Sengerema, Misungwi, Kwimba, Magu na jana ikafanyika Wilaya ya Nyamagana ambapo ziara hiyo inatarajiwa kutamatishwa katika Wilaya ya Ilemela kesho kutwa Jumanne ambapo pia Mtaturu atatembelea miradi mbalimbali ya Maendeleo katika Wilaya hiyo na kuanzia majira ya saa tisa mchana atawahutubia wananchi katika Mkutano wa hadhara utakaofanyika katika Uwanja wa Magomeni Kirumba.
Na:George GB Pazzo
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoani Mwanza Miraji Mtaturu akiwasili jana katika Viwanja vya Stand ya Igoma Jijini Mwanza huku akiwa anaendesha pikipiki yeye mwenyewe ambapo alikuwa na Mkutano wa hadhara.
"Hapo vipiiiiiiiiiii, Hapo Vipiiiiiiiiiiiiiiii".Alisikika akisema Miraji Mtaturu (Katikati) ambae ni Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza baada ya kupanda jukwaani kama ishara ya kuwasalimia wananchi waliohudhuria katika Mkutano wake jana. Kulia na Kushoto ni Wanahabari wakinasa matukio.
"Hapo Sawaaaaaaaaaa, Hapo Sawaaaaaaa". Zilikuwa ni sauti kutoka kwa wananchi waliohudhuria Mkutano wa Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu uliofanyika jana katika Viwanja vya Igoma Stand Jijini Mwanza.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza (Kulia) akiwapongeza jukwaani baadhi ya Madiwani wa CCM wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa uchapaji kazi wao mzuri.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza (Kulia) akiwapongeza jukwaani baadhi ya Madiwani wa CCM wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa uchapaji kazi wao mzuri.
Hatimae Ukawadia wasaa wa Wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Kurejesha kadi za Chama hicho na kwa ajili ya kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM ambapo walio jukwaani ni baadhi ya waliorejesha kadi za Chadema wakimkabidhi Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu kadi za Chadema. Ilielezwa kuwa zaidi ya Vijana Mia nne huku wengi wao wakiwa ni wanavyo mbalimbali kutoka Jijini Mwanza jana waliweza kurejesha kadi za Chadema na hivyo kujiunga na CCM.
Jamaa (Kulia) baada ya kukabidhi kadi ya Chadema akapewa Tshirt ya CCM na kuivaa akiwa Jukwaani.
Na ushuhuda ukatolewa na mmoja wa wanachama waliojiunga na CCM ambapo alieleza kuwa wameamua kujiunga na CCM baada ya kutambua kuwa hakuna demokrasia ya kweli ndani ya Chadema.
Hapa Mtaturu (Kushoto) akifurahia burudani iliyokua ikitolewa na mwimbaji kutoka Igogo Jijini Mwanza.
Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza Aimon Mangelepa akitoa salamu zake.
Mwenyekiti wa Chama cha Madereva Kanda ya Ziwa Dede Petro Dede (Kulia) akitoa salamu zake. Kushoto ni Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza Aimon Mangelepa.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Raphael Shiratu (Katikati) akisalimia wananchi. Kulia na Kushoto ni Wanahabari.
Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana Elias Mpanda akisalimia katika Mkutano huo.
Diwani wa Kata ya Mkolani (CCM) ambae pia ni Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula akizungumza katika Mkutano huo.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga (Mtumishi wa Mungu) akisalimia wananchi katika Mkutano huo.
Jumbe mbalimbali zilikuwepo huku zikiashiria Kudumisha Upendo ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM.
Umati mkubwa uliweza kuhudhuria Mkutano huo bila kujali itikadi za Kisiasa. Mkutano huo umeacha historia kubwa kutokana na namna ambavyo wananchi walivyojitokeza kwa wingi.
CREDIT:RADIO METRO FM.

No comments:

Powered by Blogger.