LIVE STREAM ADS

Header Ads

SIASA ZA CHUKI NA MAUAJI HAZIKUBALIKI KAMWE.

Mmoja wa Waigizaji kutoka Igogo Jijini Mwanza akiigia jana katika Mkutano wa Chama cha Mapinduzi CCM uliofanyika Stand ya Igoma Jijini Mwanza ambapo Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza alikuwa akiwahutubia wananchi na wana-CCM.
Igizo hilo lilivuta hisia za watu wengi kutokana na kuelezea namna ndugu, jamaa na marafiki wanavyouana wenyewe kwa wenyewe kutokana na tofauti zao za Kisiasa jambo ambalo si sahihi.
Waigizaji walijaribu kuwakanya baadhi ya wanasiasa wanaohamasisha chuki na mauaji kwa wapinzani wao.
Na:George GB Pazzo
Baadhi ya waigizaji kutoka kundi la sanaa lililopo Igogo Jijini Mwanza wakitoa igizo lao jana katika Mkutano wa CCM uliofanyika katika Viwanja vya Stand ya Igoma Jijini Mwanza.
Pichani wanaonekana waigizaji waliochukua uhusika wa wahanga wa ghasia za Kisiasa ambao asilimia kubwa huwa ni wanawake na watoto.
Hakika Siasa za Chuki na Mauaji hazifai ndugu zangu Watanzania hivyo tuwe makini na baadhi ya wanasiasa wasio na mapenzi mema na sisi wapiga kura wao hivyo Itikadi za Kisiasa zisisababishe ndugu kwa ndugu tuuane.
BINAGI MEDIA GROUP PRODUCTIONS

No comments:

Powered by Blogger.