LIVE STREAM ADS

Header Ads

WATENDAJI WA SERIKALI JIJINI MWANZA WAONYWA.

Baadhi ya Watendaji kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakiwa katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Nyamagana kabla ya kwenda katika Ukaguzi wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo katika Wilaya hiyo ikiwa ni katika Ziara ya Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu.
 Na:George GB Pazzo
Watendaji wa Serikali katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza wametakiwa kusimamia vyema majukumu yao ikiwa ni pamoja na kutojihusisha na itikadi za kisiasa katika kutekeleza majukumu yao.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Mwanza Miraji Mtaturu alitoa kauli hiyo mapema jana katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Nyamagana, kabla ya kuelekea katika Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo ili kujionea namna Ilani ya Chama hicho ya mwaka 2010/15 inavyotekelezwa.

Mtaturu alibainisha kuwa Mtendaji yeyote wa Halmashauri atakaebainika kuwa anakwamisha shughuli za Maendeleo katika eneo lake kutokana na itikadi za kisiasa, atachukuliwa hatua kali ikiwemo kutimuliwa kazini.

Kauli ya Mtaturu imejili huku kukiwa na taarifa kuwa baadhi ya Watendaji katika Halmashari mbalimbali Mkoani Mwanza, wanakwambisha baadhi ya miradi ya Maendeleo kutokana na utashi wao wa Kisiasa kwa lengo la kuzua lawama kutoka kwa wananchi dhidi ya Serikali iliyoko madarakani ya Chama cha Mapinduzi CCM.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Katikati) akifuatilia kwa umakini taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama hicho Wilaya ya Nyamagana Raphael Shiratu na Kulia ni Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana Elias Mpanda.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Katikati) akizungumza katika Kikao cha Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama hicho Wilaya ya Nyamagana Raphael Shiratu na Kulia ni Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana Elias Mpanda.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Baraka Konisaga (Aliesimama) akisoma taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi katika Wilaya yake.Kutoka kushoto ni Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Mkoa wa Mwanza Simon Mangelepa, Mwenyekiti wa Chama hicho Wilaya ya Nyamagana Raphael Shiratu, Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu na wa mwisho ni Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana Elias Mpanda.
Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza.
Credit:Radio Metro

No comments:

Powered by Blogger.