LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWANAMZIKI CHE MUNDUGWAO AFARIKI DUNIA. DR TONNY WA RADIO METRO AELEZA ANAVYOMKUMBUKA.

Mwanamuziki Chigwele Che Mundugwao enzi za Uhai wake.
Na:George GB Pazzo
Mwanamziki Mkongwe wa nyimbo za asili nchini Chigwele Che Mundugwao amefariki dunia hii leo akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili akikokuwa amelazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Che Mundugugwao amefariki dunia hii leo majira ya saa kumi na mbili asubuhi ambapo taarifa zimeeleza kuwa chanzo cha kifo chake ni maradhi ya shinikizo la damu yaliyokuwa yakimkabili.
Mwanamziki huyo ambali enzi za uhai wake alijipatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchini kupitia nyimbo zake mbalimbali ambazo ni pamoja na wimbo maarufu wa Kila Munu awe na kwao amefariki dunia akiwa na Umri wa Miaka 47 ambapo alizaliwa mwaka 1968.

Che mundugwao alijipatia umaarufu mkubwa kupitia nyimbo zake kiasi hali iliyopelekea kupata mialiko mingi katika nchi mbalimbali duniani zikiwezo Scanavia ambako alikuwa na wapenzi wengi waliokuwa wakifuatilia muziki wake.

Alphonce Tonny Kapela a.k.a Dr.Tonny ambae ni Mtangazaji wa Radio Metro Mwanza amemwelea Che Mundugwao kama msanii ambae mchango wake katika muziki uliweza kuwavutia watu wapenzi mbalimbali wa muziki wakiwemo wanamuziki kama Vile Shaa ambae aliwahi kutumia maneno ya Wimbo wake wa Kila Munu awe na kwao.

Dr.Konny anasema kuwa ni vyema tunakumuombea Che Mundugwao ili apumzike kwa amani kwa kuwa alikuwa ni chachu ya Muziki wa asili hapa nchini, ambapo anasema kuwa kwa mara ya kwanza wakati wanakutana alibaini kuwa mwanamuziki huyo mbali ya kwamba alikuwa akifanya muziki wa asili lakini pia hata mavazi yake pamoja na mwonekano wake ulikuwa ni wa Kiafrika zaidi.
BONYEZA PLAY KUMSIKILIZA DR.TONNY KUPITIA BINAGI RADIO

Alphonce Tonny Kapela a.k.a Dr.Tonny kutoka Radio Metro Fm Mwanza
BINAGI MEDIA GROUP PRODUCTION

No comments:

Powered by Blogger.