LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWENYETI WA UWT SAUT JIJINI MWANZA ASEMA WANAFUNZI WA VYUONI HAWATUMIKI KISIASA.

Baadhi ya Vijana wa Kike kutoka Shule ya Sekondari ya Alliance ya Jijini Mwanza wakiwa pamoja na Vinaja wengine wa Kike kutoka Vyuo mbalimbali Jijini Mwanza wakiimba na Kufurahia na baadhi ya Viongozi wa UWT Mkoani Mwanza katika Kongamano la Vijana wa Kike lililofanyika jana katika Ukumbi wa Gandh Hall Jijini Mwanza lililoandaliwa na Umoja wa Wanawake Tanzania kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine Mwanza.
 Na:George GB Pazzo
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine SAUT Mkoani Mwanza, amepingana na shutma zinazoelekezwa kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu hapa nchini kuwa wanatumika kisiasa na baadhi ya wanasiasa.

Jesca Mbogo ambae ni Mwenyekiti wa Umoja huo alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akizungumza na Radio Metro Fm ya Jijini Mwanza, wakati wa Kongamano la Vijana wa Kike lililoandaliwa na Umoja huo lililofanyika katika Ukumbi wa Gandh Hall Jijini Mwanza.

“kiongozi wa chama cha kisiasa anapohitaji ufanye jambo Fulani maana yake ni kwamba anahitaji ufanye jambo hilo kwa ajili ya maslahi ya chama hivyo haina maana kuwa anakutumia kisiasa”.Alisema Mbogo.
Aidha Mbogo alibainisha kuwa siasa za vyuoni hufanyika nje ya chuo hivyo jamii isiwe na imani kwamba wanavyuo kujihusisha na siasa kunaweza kuvuruga mstakabali wa masomo yao.


Kuhusiana na Kongamano hilo, Mbogo alibainisha kuwa lengo lake lilikuwa ni kuwakusanya kwa pamoja vijana wote wa kike na kuwapa semna juu ya masuala mbalimbali ambayo ni pamoja na maadili na fursa nyingi wanazoweza kuzipata wakiwa ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM ambapo pia aliwasihi vijana wote kujiunga na chama hicho kwa kuwa ndicho chama pekee cha kisiasa hapa nchini kinachotoa fursa kwa vijana kwa ajili ya kuzungumzia masuala yao.
Baadhi ya Vijana wa Kike kutoka Shule, Vyuo pamoja na Kata mbalimbali Jijini Mwanza wakiimba na kufurahia katika Kongamano la Vijana lililofanyika jana katika Ukumbi wa Gandh Hall Jijini Mwanza.
Baadhi ya Vijana na akina mama waliohudhuria Kongamano la Vijana lililofanyika jana katika Ukumbi wa GandhHall Jini Mwanza.
Baadhi ya Vijana na akina mama waliohudhuria Kongamano la Vijana lililofanyika jana katika Ukumbi wa GandhHall Jini Mwanza.
Baadhi ya Vijana na akina mama waliohudhuria Kongamano la Vijana lililofanyika jana katika Ukumbi wa GandhHall Jini Mwanza.
Jesca Mbogo (Kulia) ambae ni Mwenyekiti wa UWT SAUT akizungumza na GB Pazzo (Kushoto) kuhusu kongamano la Vijana lililofanyika jana katika Ukumbi wa Gandh Hall Jijini Mwanza. Kongamano hilo liliandaliwa na UWT SAUT kwa lengo la kutoa elimu mbalimbali hususani kuwajenga kukua katika siasa safi kwa mstakabali wao wa baadae kisiasa.
CREDIT: RADIO METRO

No comments:

Powered by Blogger.