LIVE STREAM ADS

Header Ads

UJUMBE WA IMETOSHA FOUNDATION WATUA KANDA YA ZIWA KWA SHUGHULI MAALUMU.

Ujumbe wa Kampeni ya Imetosha Kutoka IMETOSHA FOUNDATION ukiwa katika picha ya Pamoja na Staffs wa Radio Metro Jijini Mwanza hii leo baada ya kipindi cha Pambazuko la Metro Fm ambapo walikuwa wakielezea masuala mbalimbali yanayofanywa na IMETOSHA FOUNDATION katika kukomesha Mauaji ya Watu wenye ulemavu wa Ngozi hapa nchini pamoja na Ujio wa Ujumbe huo katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa.
                               Picha na Mkala Fundikira-Mjumbe Imetosha Foundation
Ujumbe wa Imetosha Foundation ambao unaendesha Kampeni ya Imetosha iliyolenga kutokomeza Mauaji kwa Watu wenye Ulemavu wa ngozi nchini, Umetua Jijini Mwanza kwa lengo kukutana na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiewemo wa Ulinzi na Usalama katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Mwenyekiti wa Imetosha Foundation Masoud Kipanya amesema kuwa lengo la ujio wao katika Mioa ya Kanda ya Ziwa ni kukutana na Viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na Ulinzi na Usalama kwa ajili ya kujitambulisha kwao kabla ya kuanza kufanya mikutano mbalimbali katika Mikoa hiyo yenye lengo la kuzuia mauaji kwa watu wenye ulemavu wa ngozi nchini.

Kipanya amesema kuwa Ujumbe huo umekusudia kukutana na Wakuu wa Mikoa, Wilaya pamoja na Makamanda wa Polisi ambapo kwa kuanza wanatarajia kukutana na Viongozi wa Mkoa wa Mwanza kabla ya kuelekea Shinganya pamoja na Mikoa mingine ya Kanda ya Ziwa.

Mbali na Kipanya ujumbe huo umeambatana na wajumbe wengine ambao ni Mkala Fundikira, Kelvina John Wakuvwanga, Jhikoman ambapo mwenyeji wao Jijini Mwanza ni Juma Herman ambae ni Meneja Green Palm Hotel.
Mwenyekiti wa Imetosha Foundation Masoud Kipanya (Kulia) akiwa pamoja na Wakuvwanga (kushoto) ambae ni Mjumbe wa Imetosha pamoja na Rosier (Katikati) kutoka Radio Metro.
Mwenyekiti wa Imetosha Foundation Masoud Kipanya (Kulia) akiwa pamoja na Jhikoman (kushoto) ambae ni Mjumbe wa Imetosha Foundation pamoja na Rosier (Katikati) kutoka Radio Metro.
Mwenyekiti wa Imetosha Foundation Masoud Kipanya (Kulia) akiwa pamoja na Kelvina John (kushoto) ambae ni Mjumbe wa Imetosha pamoja na GB Pazzo (Katikati) kutoka Radio Metro na C.E.O wa Mtandao huu.
Juma Herman (Kulia) ambae ni Meneja wa Green Palm Hotel ya Jijini Mwanza akiwa pamoja na GB Pazzo (Kutosho) kutoka Radio Metro na C.E.O wa Mtandao huu.
CREDIT:Radio Metro

No comments:

Powered by Blogger.