NIYONZIMA KUUKOSA MCHEZO DHIDI YA YANGA NA ETOILE DU SALEH JUMAMOSI.
Genya Richard Mchambuzi wa Michezo
Na:Genya
Richard
Kiungo
mahiri wa klabu ya yanga Haruna Niyonzima amezuwa wasiwasi mkubwa klabuni hapo
baada ya kuwepo taarifa kuwa kiungo huyo huenda akaukosa mchezo kati ya timu na
Etoile du Sahel kutoka nchini Tunisia katika mchezo wa kombe la shirikisho
barani Afrika siku ya jumamosi katika uwanja wa Taifa Jijin Dar es laam unaotarajiwa
kuchezwa majira ya saa tisa alasiri.
Daktari wa misuli katika klabu hiyo Jackobo Onyango ambaye alitumia muda wa dakika kumi
kumtibu misuli Niyonzima alisema kuwa hali ya Mchezaji huyo inaendelea vyema na
kuna uwezekano mkubwa wa kucheza mechi hiyo siku ya jumamosi.
Wakati
huo huo tayari Watunisia hao wameisha wasili nchini kwa ajili ya pambano hilo
ambapo msemaji wa klab hiyo ya Etoile du Sahel Musitafa amesema kuwa timu hiyo
imejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo huo huku akisisitiza kuwa lazima Yanga
ikione cha mtema kuni siku ya pambano hilo.
HISTORIA YA
ETOILE du SAHEL
Ikumbukwe
kuwa Etoile du Sahel ni timu kongwe hapa Barani Afrika kwani ilianzishwa May 25 mwaka 1920 na mpinzan
wake mkuu ni timu ya Espearance du Sportivu. Etoile imeisha chukua kombe la
shirikisho barani Afrika kwa miaka miwili ambapo mara ya kwanza kuchukua kombe
hilo ilikuwa mwaka 1997 na mara ya pili ikiwa ni mwaka 2003.
Mwaka
1950 klabu hii ilichukua ubingwa wa ligi ya Tunisia kwa mara ya kwanza ambapo tayari ambapo
imekwisha nyakua ubingwa wa ligi hiyo mara tisa huku sifa kubwa ya timu hiyo
ikiwa ni kujua kupoteza muda pindi inapokuwa uwanjan kwani hutumia asilimia zaidi
ya 50 kucheza na waamuz kisaikolojia kwa kulalama na kumtaka refa kutoa adhabu
iwe penati ama faulu.
Pia ni wapigaji wazuri wa mipira iliyokufa
[balldied] ambapo Waarabu hao hutumia asilimia zaidi ya 20 kucheza mpira
uwanjan kwa dakika 60 ama 70 kwa kucheza mchezo ambao ni viding game yaan
wakiwa ni watu wanaopenda kujirusha sana tena wakitumia ujanja wao kumtaka refa
kuwabeba .
Hivyo
Yanga inawabidi kuwa makini na Waarabu hao ambao wanajua sana fitina katika
soka na inabidi Yanga siku hiyo icheze nao kisaikolojia vinginevyo safari yao
itabaki kuwa hadithi ya soka la Tanzania kuwa “tutajipanga msimu ujao tena tukionekana
kuwatupia lawama waamuzi ama ubovu wa viwanja”.
USHAURI: genyarichard@gmail.com
0713208878
BINAGI MEDIA GROUP PRODUCTION
No comments: