LIVE STREAM ADS

Header Ads

WALIA NA MAMLAKA ZA USIMAMIZI WA CHAGUZI KWA KUVURUGA AMANI NA USALAMA.

Washiriki wa Mdahalo wa Uchaguzi uliofanyika jana Jijini Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja.
 Na:George GB Pazzo
Mamlaka zinazohusika katika usimamizi wa chaguzi mbalimbali hapa nchini zimetakiwa kutumia busara katika utekelezaji majukumu yake wakati wa Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu lengo likiwa ni kufanikisha uchaguzi huo kufanyika kwa Amani na Usalama.

Hayo yalielezwa na baadhi ya Washiriki wa Mdahalo wa Uchaguzi uliyofanyika jana Jijini Mwanza, ukiwa umelenga kujadili masuala mbalimbali yahusuyo Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu ambayo ni pamoja na Viashiria vya vurugu na uvunjifu wa amani nchini.

Washiriki hao walieleza kuwa Mamlaka husika za Usimamizi wa Uchaguzi ambazo ni pamoja na Tume ya Taifa ya Uchaguzi pamoja na Jeshi la Polisi, zinapaswa kusimamia vyema utekelezaji wa majukumu yake kwa kuwa mamlaka hizo mara kadhaa zimekuwa zikishindwa kutekeleza vyema majuku yake na hivyo kuzua vurugu katika chaguzi mbalimbali zilizopita.

Nae Jimmy Luhende ambae ni Kiongozi wa Taasisi ya kufuatilia Demokrasia na Utawala Bora nchini ambayo ndiyo imeandaa Mdahalo huo, alisema kuwa taasisi hiyo imejipanga kufanya midahalo mbalimbali juu ya uchaguzi hapa nchini ambayo imelenga kuhakikisha kuwa kunakuwepo na mwamko wa wananchi kujitokeza na kushiriki zoezi la upigaji kura kwa Imani na Amani bila kuwepo hofu yoyote inayoashiria uvunjifu wa amani.

Aidha alisisitiza kuwa taasisi hiyo kupitia midahalo yake ya uchaguzi ambayo tayari imeanza kufanyika hapa nchini, imelenga kuhakikisha kuwa inawahamasisha wanachama wa vyama vya siasa kuhudhuria mikutano ya kampeni za kisiasa ya vyama tofauti tofauti bila kuwepo kwa hofu yoyote ya utengano wa itikadi za kisiasa.

Wanau mbalimbali waliohudhuria Mdahalo huo  ni pamoja na Viongozi wa Kisiasa, Kidini, Jeshi la Polisi, Mtandao wa Utetezi wa Haki za Binadamu nchini, Wanahabari, Wanafunzi, wananchi pamoja na wadau wengine kutoka mashirika na taasisi mbalimbali za serikali na zisizo za serikali.
Washiriki wa Mdahalo wakiwa katika picha ya pamoja
Bituro Kazeri ambae ni Afisa Habari TASAJA akizungumza na wanahabari
Yasmin Simba ambae ni Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza akizungumza na wanahabari wakati wa Mdahalo.
Onesmo Olengurumo kutoka Tume ya Haki za binadamu na Utawala Bora akizungumza na Wanahabari katika Mdahalo huo.
Pendo Ogijo (Kushoto) ambae ni Mwenyekiti wa Muda ACT Wazalendo Mkoani Mwanza akizungumza na GB Pazzo (Kulia).
Kushoto ni Adrian Tizeba ambae ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mwanza akizungumza na wanahabari.
Jimmy Luhende (Kushoto) ambae ni Kiongozi wa Taasisi ya kufuatilia Demokrasia na Utawala Bora nchini akizungumza na GB Pazzo (Kulia).
BINAGI MEDIA GROUP PRODUCTION

No comments:

Powered by Blogger.