LIVE STREAM ADS

Header Ads

BINAGI RADIO HABARI: MUUNGANO WA MACHINGA MKOA WA MWANZA WAMLILIA RAIS KIKWETE.

Mwenyekiti wa Uongozi Mpya ambao uliingia madarakani mwezi wa Kwanza Mwaka huu wa Muungano wa Machinga Mkoa wa Mwanza Said Tembo akizungumza na Wanahabari jana katika Ukumbi wa Florida Resort Jijini M wanza baada ya uongozi huo kukutana na wanachama wake kwa ajili ya kuelezea masuala mbalimbali yaliyotekelezwa na uongozi huo katika kipindi cha siku 83 tangu kuingia kwake madarakani lakini pia kueleza masuala mbalimbali yanayotarajiwa kutekelezwa katika kipindi kingine kijacho.
 Na:George GB Pazzo
Muungano wa Machinga Mkoa wa Mwanza umemlilia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Mrisho Kikwete, kuwasaidia upatikanaji wa Mitaji kwa ajili ya kuwawezesha kukuza biashara zao.

Kilio cha Machinga hao kilitolewa jana na Katibu Mkuu wa Muungano huo Moshi Maketa na Kuungwa mkono na Wajumbe wote, katika Mkutano wa Muungano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Florida Hotel.

Maketa alibainisha kuwa asilimia kubwa ya Machinga Mkoani Mwanza wana mitaji ya inayoanzia kati ya shilingi Elfu Kumi hadi shilingi Elfu Hamsini kiasi ambacho alisema hakikidhi mahitaji yao, hivyo ni vyema Serikali kupitia Rais Kikwete ikawawezesha kupata mtaji wa fedha usiopungua Milioni Mia Tano kwa ajili ya Kukopeshana na hivyo kuinua biashara zao.

Mwenyekiti wa Muungano huo wa Machinga Mkoa wa Mwanza Said Tembo alibainisha kuwa awali machinga Jijini Mwanza walikuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa maeneo ya kufanyia biashara, lakini baada ya uongozi wake kuingia madarakani changamoto hiyo imeweza kushughulikiwa ikiwa ni kwa ushirikiano wa karibu na Viongozi wa Serikali katika ngazi ya Mkoa na Halmashauri ya Jiji huku pia akipongeza ushirikiano uliopo katika Machinga na Mgambo wa Jiji jambo ambalo alisema limesaidia kuleta utulivu baina ya machinga na Mgambo wa Jiji.

Alisema kwa hivi sasa changamoto kubwa ambayo Muungano huo unapambana nayo ili kuhakikisha kuwa inatatuliwa ni ukosefu wa Mitaji kwa ajili ya Machinga ambapo nae alisisitiza juu ya kauli iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Muungano huo (Moshi Maketa) ya Kuiomba Serikali kuwawezesha Mitaji kwa ajili ya Kuimarisha biashara zao.

Nae Mazinge Hussein ambae ni Katibu Mkuu idara ya Maafa ndani ya Muungano huo aliwasihi Machinga Mkoani Mwanza kurudisha imani kwa uongozi mpya ulioingia madarakani tangu mwezi januari mwaka huu na hivyo kuondoa hofu iliyokuwepo awali ambapo machinga walikuwa hawashiriki shughuli mbalimbali ikiwemo kusaidiana katika maafa mbalimbali kutokana na uongozi uliokuwepo awali kutumia nafasi hiyo kwa ajili ya manufaa binafsi.

Kwa upande wake Maneno Juma ambae ni Machinga anaefanya shughuli zake katika eneo la Sahara aliupongeza Uongozi mpya ulioko madarakani kwa namna ambavyo uongozi huo umejitahidi katika kuwatafutia machinga maeneo kwa ajili ya kufanyia biashara zao ambapo alitoa rai kwa uongozi huo kuendelea kutafuta maeneo mengine kwa ajili ya machinga huku pia akisisitiza kuwa changamoto ya ukosefu wa mitaji inayowakabili machinga inapaswa kuendelea kutafutiwa ufumbuzi.

Mkutano huo ulikuwa ulilenga juu ya Uongozi mpya wa Muungano huo wa Machinga Mkoa wa Mwanza unaoongozwa na Mwenyekiti wake Said Tembo ambao uliingia madarakani tangu mwezi wa kwanza mwaka huu, kuelezea mafanikio yake kadhaa yaliyotekelezwa katika kipindi cha siku 83 zilizopita pamoja na kueleza masuala ambayo yanatarajiwa kutekelezwa katika kipindi kijacho.

Miongoni mwa Mafanikio yaliyoelezwa kutekelezwa na Muungano huo ni pamoja na kufanikiwa kupata maeneo rasmi kwa ajili ya machinga kufanyia biashara zao Jijini Mwanza sanjari na kufanikiwa kujenga Stoo ya kisasa kwa ajili ya Machinga kutunzia mizigo yao katika eneo la Sahara huku matarajio ya baadae yakiwa ni Muungano huo kuanzisha Timu ya Mpira wa Miguu itakayofahamika kwa jina la Machinga United Football Club lakini pia Kushiriki katika shughuli za uwekezaji katika sekta ya Kilimo na Uvuvi.
SIKILIZA BINAGI RADIO HAPA CHINI.

Mwenyekiti wa Muungano wa Machinga Mkoa wa Mwanza Said Tembo akizungumza katika Mkutano wa Muungano huo uliofanyika jana katika Ukumbi wa Florida Resort Jijini Mwanza.
Katibu Mkuu wa Muungano wa Machinga Mkoa wa Mwanza Moshi Maketa akizungumza katika Mkutano wa Muungano huo uliofanyika jana katika Ukumbi wa Florida Resort Jijini Mwanza.
David James ambae ni Katibu Msaidizi wa Muungano wa Machinga Mkoa wa Mwanza Moshi Maketa akizungumza katika Mkutano wa Muungano huo uliofanyika jana katika Ukumbi wa Florida Resort Jijini Mwanza.
Jamal Said ambae ni Mweka Hazina wa Muungano wa Machinga Mkoa wa Mwanza Moshi Maketa akizungumza katika Mkutano wa Muungano huo uliofanyika jana katika Ukumbi wa Florida Resort Jijini Mwanza.
Wajumbe wa Muungano wa Machinga Mkoa wa Mwanza wakiwa katika Mkutano wao uliofanyika jana Florida Resort Jijini Mwanza.
Wajumbe wa Muungano wa Machinga Mkoa wa Mwanza wakinyoosha Mikono juu kama ishara ya kuunga mkono kauli ya mwenyekiti wao ya Kuomba Serikali kuwasaidia mitaji kwa ajili ya kukuza biashara zao.
Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari.
BINAGI MEDIA GROUP PRODUCTION

No comments:

Powered by Blogger.