LIVE STREAM ADS

Header Ads

UCHAMBUZI: MAKOCHA WANNE WANAOTISHA HIVI SASA UEFA.

Genya Richard ambae ni Mchambuzi wa Michezo Radio Metro na Binagi Media Group.
Na: Genya Richard
Ni makocha wanne tu ambao walikuwa wachezaji katika kikosi cha timu ya Barcelona mwaka 1996 wametisha baada ya timu zao kuingia hatua ya robo final  ya Ligi ya mabingwa. Na wakati makocha hao wakiwa wachezaji kocha wao alikuwa ni Bobby Robbson raia wa Uingereza kwa sasa ni marehem na msaidiz wake alikuwa ni Jose Mourinho.

Makocha hao ni
1.JULLEN LEPETEGU; Kwa sasa ni kocha wa klab ya FC PORTO na leo hii timu yake itapambana na timya Buyern Munich pambano ambalo likuwa na mvuto wake na lolote linaweza kutokea mana wawili wanafahamiana vizuri ikiwa walisha kucheza pamoja,japo wengi waipa nafas buyern lakin porto ya sasa si ya mchezo ni porto iliyowahi kuchukua ubingwa ikiwa na JoseMourinho ikiwa na wakali kama McCarthy raia wa Afrika Kusin huo ulikuwa mwaka 2004-2005 ambapo porto iliweka rekod ya kuchukua ubingwa toka ilivyofanya mwaka 1993
   
2. PEP GUARDIOLA; Kwa sasa nikocha wa klab ya Buyern Munich ambaye leo timu yake itashuka uwanjan kumenyana na timu fc Puorto ni pambano ambalo litakuwa ni la kukata na shoka kutokana na ubora wa vikosivya timu zote mbili

3.LUIS ENRINQUE;Kwa sasa ni kocha wa tim ya Barcelona na kwa siku ya leo timu yake itakuwa na kibarua dhidi ya timu ya PSG ambapo wawilI hao wajuana vizuri tangu enzi wakiwa wachezaji watimu ya Barcelona leo tena wanakutana ikiwa walikuwa wote kwenye hatua ya makundi.

4.LAURENT BLANC;Kwasasa ni kocha watimu ya PSG ambapo leo hii timu yake itakuwa uwanjani kucheza  na Barcelona, ukiangalia kwa umakin mechi za leo zitakuwa na mvuto wa aina yake kutokana na makocha wote kufahamiana vizuri.

Na hao ndio makocha wanne wanaotisha Club Bingwa Barani Ulaya UEFA ambao ni zao la Barcelona...Jiunge nasi wakati mwingine kwa uchambuzi zaidi wa Kimichezo.
                                          BINAGI MEDIA GROUP PRODUCTION

No comments:

Powered by Blogger.