LIVE STREAM ADS

Header Ads

YANGA YAWEKA MAMBO HADHARANI LIGI KUU TANZANIA BARA.

Na:Genya Richard
Hatimaye kile kitendawili cha nani atakuwa bingwa wa msimu wa mwaka 2014/2015 kimeteguliwa kwa kushuhudia klabu ya Yanga kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara maarufu kama Vodacom Premier League na kulipeleka katika makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani,yalipo makao makuu ya klabu hiyo, likitokea Chamanzi Mbande yalipo maskani ya Azam fc waliokuwa Mabingwa wa Kombe hilo msimu uliopita.

Yanga Sc imeivua ubingwa Azam kufuatia ushindi wa wa mabao 4-1 dhidi yaPolisi Moro mchezo uliyopigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar hivyo kufikisha jumla ya point 55 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote katika ligi hiyo.

Kocha wa timu ya Yanga Hans van der Pluijm na msaidizi wake Charles BonphaMkwasa walionekana kuwa na furaha baada ya vijana wa Jangwani kucheza soka safi na la kuvutia na kupata ushindi munono.

Kwa Yanga hili linakuwa ni taji la 25 la Ligi Kuu kwa Yanga baada ya kulitwaa katika miaka ya 1968, 1969, 1970, 1971, 1974, 1981, 1983, 1985, 1987, 1989, 1991, 1992, 1993, 1996, 1997, 1998, 2002, 2005, 2005, 2006, 2008, 2009, 2011, 20013 na 2015.

Baada ya mechi hiyo shangwe na vigeregere vya ubingwa vilitawala uwanja mzima hata hivyo hali kama hii haikutokea Dar pekee bali hata katika mikoa ya mbalimbali ya ya Bara na visiwani,mashabiki wa Yanga wameshehekea ubingwa huo.


Hata hivyo vita mebakia katika nafasi ya pili kwani kuna vita kali kati ya Simba na Azam ambapo Azam anashika nafasi ya pili akiwa na pointi 45 huku akiwa amebakiza michezo 3 na Simba anashika nafasi ya tatu akiwa na pointi 41 akiwa na michezo miwili.

No comments:

Powered by Blogger.