LIVE STREAM ADS

Header Ads

MANISPAA YA ILEMELA MKOANI MWANZA HALI SI SHWARI. YAPEWA SIKU 30 KUWEKA MAMBO SAWA.

Hali ya Miundomindu katika Halmashauri ya Manispiaa ya Ilemela Mkoani Mwanza hailizishi hali ambayo imesababisha Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu kutoa Siku 30 miundombinu hiyo iwe imerekebishwa haraka iwezekanavyo ili kuondoa adha kwa wananchi lakini pia maafa yanayoweza kutokea wakati wowote husani wakati wa Mvua.
Na:George GB Pazzo
Mtaturu aliekuwa katika ziara ya Kukagua Miradi ya Maendeleo katika Manispaa hiyo jana alijionea hali mbovu ya Miundombinu katika eneo la Kilimahewa ambapo daraja la Ujiji limeweza kusombwa na maji ya Mvua inayoendelea kunyesha Mkoani Mwanza na hivyo kuhatarisha maisha ya wananchi wakiwemo wanafunzi wa shule za msingi wanaotegemea daraja hilo linalopitisha maji ya Mto Msuka kwenda Ziwa Victoria.
Ziara ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza ikiwa ikiwa Kilimahewa kujionea namna mbiunombinu ilivyoharibika katika eneo hilo ambapo alitoa muda wa siku 30 iwe imerekebishwa.
Ziara ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu ikijionea hali ya Daraja la Kwa Msuka ambalo wakati wa Mvua Maji hujaa na kupita juu ya daraja na hivyo kusababisha adha kubwa kwa watumiaji wake huku pia maji yakisambaa ovyo na kuelekea katika nyumba za wananchi. Katika daraja hili Mhandisi wa Barabara wa Manispaa ya Ilemela Mikidadi Adam alibainisha kuwa ndani ya Miezi mitatu kero iliyopo itakuwa imetatuliwa ambapo daraja litajengewa kingo za kuzuia maji kuzagaa ovyo pamoja na kuongeza upana wake ili kuzuia maji kupita juu ya daraja.
Ziara ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu ikijionea hali ya Daraja la Kwa Msuka ambalo wakati wa Mvua Maji hujaa na kupita juu ya daraja na hivyo kusababisha adha kubwa kwa watumiaji wake huku pia maji yakisambaa ovyo na kuelekea katika nyumba za wananchi. Katika daraja hili Mhandisi wa Barabara wa Manispaa ya Ilemela Mikidadi Adam alibainisha kuwa ndani ya Miezi mitatu kero iliyopo itakuwa imetatuliwa ambapo daraja litajengewa kingo za kuzuia maji kuzagaa ovyo pamoja na kuongeza upana wake ili kuzuia maji kupita juu ya daraja.
Wanafunzi wakipata adha ya kupita katika eneo la Kilimahewa Wilayani Ilemela baada ya Barabara inayotoka eneo la Ujiji kuharibika kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha Mkoani Mwanza.
Hii ni barabara na si dampo....Ziara ya katika wa CCM Mkoa wa Mwanza ikielekea katika daraja la Ujiji kujionea hali halisi.
Eng.Mikidadi Adam (Kushoto) Mhandisi wa Barabara Manispaa ya Ilemela akielezea mipango ya kurekebisha hali ya Miundombinu katika Manispaa hiyo ambapo alisema kuwa ndani ya Miezi Mitatu ijayo hali itakuwa shwari kabisa. Kulia ni Mwenyeki wa CCM Wilaya ya Ilemela Nelson Mesha.
Abely Saguda Pyagu ambae ni Mwenykiti Mtaa wa Nyamanoro C (Chadema) akielezea adha wanayoipata kutokana na Ubovu wa Miundominu katika Mitaa yote ya Kilimahewa. Aliimboa Manispaa ya Ilemela kuharakisha ukarabati wa Miundombinu hiyo huku akiahidi kuwasiliana na Mbunge wa Jimbo la Ilemela Highness Kiwia (Chadema) ili kutoa Ushirikiano wake katika zoezi hilo ambapo aliiambia Binagi Media Group kuwa Mbunge huyo alipaswa kushiriki katika ziara ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu ili kwa pamoja kutafuta suluhisho kwa changamoto zilizopo bila kujali itikadi za kisiasa kwa kuwa yeye ni kiongozi wa wananchi wote.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza Manju Msambya (Mwenye Suti) akisalimiana na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Katikati) baada ya kuwasili katika Ofisi za Manispaa ya Ilemela kwa ajili ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo ikiwa ni katika kujionea utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2010/15.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Kushoto waliokaa) na Viongozi wengine wa Chama wakisaini kitabu cha wageni baada ya Kuwasili katika Ofisi za Manispaa ya Ilemela.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (aliesimama) akizungumza na Watumishi na Watendaji wa Manispaa ya Ilemela baada ya kuwasili katika Manispaa hiyo jana. Zaidi alitoa muda wa mwezi mmoja kwa watendaji wa barabara kuhakikisha kuwa Barabara ya Busweli iwe imerekebishwa baada ya kuwa katika hali mbaya jambo linaloleta adha kwa watumiaji wake.
Viongozi na Makada wa CCM Mkoa wa Mwanza.
Katibu wa CCM Wilaya ya Ilemela Loth Olelemeirut (Kulia) akiwa pamoja na Diwani wa Kata ya Bugogwa (CCM) na Naibu Meya wa Manispaa ya Ilemela Dede Swila Dede (Kulia).
Baadhi ya Watumishi na Watendaji wa Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza wakifurahia Maneno ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (hayuko pichani).
Ziara ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza ikikagua ujenzi wa Jengo la CCM Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza lililopo Mtaa wa Kigala Kata ya Busweli Wilayani humo.
Ziara ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu ikikagua ujenzi wa Jengo la CCM Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza lililopo Mtaa wa Kigala Kata ya Busweli Wilayani humo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza akisalimiana na Makada wa Chama baada ya Kuwasili katika Ofisi za Chama hicho Kata ya Busweli kwa ajili ya Kujionea Ujenzi wa Vitega Uchumi vya Chama hicho Kata ya Buswelu.
Moja ya Jengo la Maduka ambalo ni Kitega Uchumi cha Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Buswelu Wilayani Ilemela Mwanza.
Jengo la Kitega Uchumi la Chama cha Mapinduzi Kata ya Busweli Ilemela Mkoani Mwanza
Ziara ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza ikielekea katika Ukaguzi wa zoezi la Ujenzi wa Maabara katika Shule ya Sekondari Nyamanoro Wilayani Ilemela.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Nyamanoro Mwalimu Praxeda Kaijage akitoa taarifa ya Ujenzi wa Maabara katika Shule hiyo ambapo alisema kuwa maboma kwa ajili ya maabara hizo yamekwisha kamilika hivyo hatua iliyopo ni ya Umaliziaji. Aliwaomba wadau kuzidi kujitokeza kuchangia ujenzi wa maabara hizo ili ziweze kukamilika kwa wakati.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (katikati) akizungumza baada ya kujionea ujenzi wa maabara katika shule ya Sekondari Nyamanoro iliyopo Ilemela Mkoani Mwanza ambapo kwa niaba ya Chama Mkoa wa Mwanza alitoa Shili Laki Tatu kwa ajili ya kusaidia katika Ujenzi wa Maabara hizo huku akiwasihi wananchi kushiriki ipasavyo katika kukamilisha ujenzi wa maabara hizo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Manju Msambya na Kulia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza Simon Mangelema.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Kushoto) akimpongeza Mkuu wa Shule ya Sekondari Nyamanoro iliypo Ilemela Mwalimu Praxeda Kaijage (Katikati) kwa namna anavyosimamia vyema zoezi la Ujenzi wa Maara katika shule yake. Kulia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza Simon Mangelema. na Mwenye suti nyuma ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela John Paul Wanga (Mwenye Suti) na kwa mbali mwenye hijabu ni mwanahabari kutoka Sahara Media Group.
Ziara ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza ikiwa katika Shule ya Sekondari Nyamanoro ili kujionea Ujenzi wa Maabara katika Shule hiyo.
Maabara tatu za masomo ya Sayansi (Biolojia, Phisicia, Chemia) katika Shule ya Sekondari Nyamanoro Wilayani Ilemela.
Ziara ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza ikiwa katika Shule ya Sekondari Nyamanoro ili kujionea Ujenzi wa Maabara katika Shule hiyo.
Ziara ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza ikiwasili katika Shule ya Sekondari Lumala kwa ajili ya Kukagua Ujenzi wa Maabara katika Shule hiyo ambapo kwa niaba ya CCM Mkoa wa Mwanza alichangia Shili Laki Tatu ili kusaidia ukamilishaji wa Maabara katika shule hiyo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akisalimiana na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Lumala Ilemela baada ya kuwasili katika shule hiyo ili kukagua ujenzi wa Maabara za Sayansi ambapo kwa niaba ya CCM Mkoa wa Mwanza alitoa shilingi Laki Tatu ili kukamilika ujenzi wa maabara hizo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela John Paul Wanga (mwenye kinasa sauti) akizungumza baada ya Ziara ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza kuwasili katika Shule ya Sekondari Lumala kwa ajili ya kujionea ujenzi wa Maabara katika Shule hiyo unavyoendelea.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Lumala wakiwa pamoja na mwalimu wao wakimsikiliza katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (hayuko pichani) baada ya kuwasili katika shule hiyo kwa ajili ya kujionea ujenzi wa Maabara unavyoendelea ambapo kwa niaba ya CCM Mkoa wa Mwanza alichangia Shilingi Laki Tatu ili kusaidia katika Ujenzi huo.
KWA UFUPI HAYO NDIYO MATUKIO YOTE YALIYOJILI JANA KATIKA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI ILEMELA KATIKA ZIARA YA KATIBU WA CCM MKOA WA MWANZA MIRAJI MTATURU AMBAPO HIYO JANA ALIHITIMISHA ZIARA YAKE WILAYANI ILEMELA YA KUTEMBELEA WILAYA ZOTE SABA ZA MKOA WA MWANZA ALIYOIANZA MARCH 22 KATIKA WILAYA YA UKEREWE.
CREDITI: BINAGI MEDIA GROU & RADIO METRO FM

No comments:

Powered by Blogger.