LIVE STREAM ADS

Header Ads

BAADA YA SSERUNKUMA KUTUPWA OUT SIMBA, WACHEZAJI WENGINE WA KIGENI KUCHOMOLEWA OUT.

Na:Genya Richard
Dani Sserunkuma ametupiwa mizigo yake na klabu ya Simba baada ya kusajiliwa na timu hiyo Desemba mwaka jana huku akiwa ameichezea mechi 17 na kufunga magoli matano timu hiyo.

Mabingwa hao wa zamani wa Tanzania na Afrika Mashariki na Kati wamemtupia virago mfungaji bora wa zamani Ligi Kuu ya Kenya, Dani Sserunkuma baada ya makubaliano ya pande zote mbili.

Mshambuliaji huyo raia wa Uganda jana aliandika katika ukurasawake wa twitter akisema kuwa amefikia uamuzi wa kusitisha mkataba wa kuendelea kuichezea timu hiyo katika musimu ujao wa Ligi Kuu bila kuweka wazi sababu zilizomfanya kuachana na timu hiyo.

Sserunkuma sasa atakuwa huru kujiunga na timu yoyote ambayo itakuwa tayari kutumia kipaji chake.Hata hivyo mchezaji huo amethibitisha kuvunja mkataba wake kupitia kwa meneja wake na maamuzi yake kuridhiwa na pande zote mbili.

Kwa upande wake Katibu mkuu waSimba Stephen Ally alithibitisha kuwa ni kweli klabu hiyo imevunja mkataba wa kuendelea kuwa na mshambuliaji huyo.

Huku katibu huyo akithibitisha kuwa kufuatia maamuzi hayo Simba haitamlipa kiasi chochote cha fedha mchezaji huyo. Ikumbukwe kuwa Sserunkuma alisajiliwa na Simba mwezi Desemba 2014 huku akipewa mkataba wa miezi 12 ambayo ilikuwa inatarajiwa kumalizika mwaka huu.

Hadi anaondoka Simba Sserunkuma aliyetokea Gor Mahia ya nchini Kenya alikuwa amecheza mechi 17 katika mashindano mbalimbali ambapo mabao matatu kati ya hayo aliyafunga katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

Bado wachezaji wengine wawili wa kigeni wamekalia sime ndani ya klabu hiyo iliyomaliza katika nafasi ya tatu katika msimu huu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara wa mwaka 2014/15.


Wachezaji hao ni Simon Sserunkuma pamoja na Joseph Owino wote wakiwa ni raia wa Uganda. Kwa upande wa Juuko Murushid na Emmanuel Okwi wao wanaendelea kujihakikishia namba katika kikosi cha Simba baada ya kufanya vizuri kwa msimu wa 2014/15 na hivyo kuendelea kuwa na uhakika wa kubaki na kikosi hicho cha Wekundu wa Msimbazi.

No comments:

Powered by Blogger.