VIONGOZI CHADEMA WATAKIWA KUWATUMIKIA WANANCHI NA SI KULALAMIKA KILA SIKU.
NA:PRISCA MSHUMBUSI MWANZA.
Katibu
wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ilemela Mkoani
Mwanza Faisali Dauda, ameutaka uongozi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo
CHADEMA kuacha tabia ya kulalamika badala yake kitimize wajibu wake wa
kuwatumikia wananchi.
Dauda alitoa kauli hiyo juzi
wakati akizungumza nasi ambapo alibainisha kuwa Chama hicho kimekuwa na
viongozi ambao kila kukicha wanaishia kuilalamikia CCM kwa kuwa ni chama
kilicho madarakani pasipo kuwa na sababu yoyote.
Alieleza kuwa katika nchi hii
hakuna hatua yoyote ya maendeleo iliyochochewa na Chadema, ambapo
alitolea mfano barabara mbovu zilizo katika Wilaya ya Ilemela ambayo mbunge
wake anatokana na Chadema.
“Barabara ya Nyampara
–Kilimahewa ni mbovu kwani wananchi wanateseka hasa kipindi cha mvua
ambapo huwa haipitiki, hivyo nashangaa wanalalamika nini? wakati wao wana
diwani na Mbunge. Alisema Dauda.
Aidha alisema kuwa, wao walikabidhiwa
madaraka na wananchi ili waweze kutatua matatizo yanayowakabili katika maeneo
yao, hivyo kama wameshindwa kutekeleza majukumu ya wananchi wao wakae pembe ili
Chama cha Mapinduzi (CCM) kiendelee kutatua matatzizo ya wananchi
wake.
“ Wasiwe kama mfano wa kikojozi,
mtu umelala nae usiku akakojoa halafu anakugeuza upande wa mkojo ili uonekane
umekojoa wewe, binafsi sikubaliani nao maana daima CCM ndio msingi imara wa
kutetea wananchi.” Aliongeza Dauda.
No comments: