LIVE STREAM ADS

Header Ads

BINAGI RADIO: CHAMA CHA MAPINDUZI CCM MKOANI MWANZA CHAANZISHA UTARATIBU HUU.

Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (katikati wenye kofia) akiwa pa moja na Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana Elias Mpanda (Kulia wenye kofia) wakiwa pamoja na washiriki wengine wa Mazoezi hii leo.
 Na:George GB Pazzo
Katika kukabiliana na Changamoto za Kiafya zinazosababishwa na Magonjwa mbalimbali, wananchi wa rika zote Jijini Mwanza wametakiwa kufanya mazoezi ya viungo kwa lengo la kujiweka katika Afya iliyo bora.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoani Mwanza Miraji Mtaturu, wakati wa Mazoezi ya Viungo yaliyoanza hii leo kwa kuwashirikisha wananchi wote chini ya Uratibu wa chama hicho.

Mtaturu amesema kuwa watu wengi wamekuwa wakipata matatizo ya kiafya huku wengine wakipoteza maisha kutokana na kutofanya mazoezi, hivyo hali hiyo si vyema ikaachwa iendelee ambapo amewasihi watu wote bila kujali rika zao kujiunga kwa pamoja kwa ajili ya Kushiriki katika Mazoezi.

Amebainisha kuwa utaratibu huo wa kufanya mazoezi ya viungo utakuwa ukifanyika kila siku ya Jumamosi kuanzia saa kumi na mbili kamili za asubuhi ambapo mazoezi hayo yatakuwa yakitanguliwa na zoezi la kukimbia ambapo mbio zitakuwa zikianzia eneo la Gand Hall Jijini Mwanza.

Miongoni mwa Walioshiriki mazoezi hayo ambao ni pamoja na Jesca Mbogo, Neema Deogratius pamoja na Ahmed Waziri Gao ambae ni Mwenyekiti wa Timu ya Soka ya Toto Africa ya Jijini Mwanza, wamekipongeza Chama cha Mapinduzi CCM kwa kuanzisha utaratibu huo wa Kufanya Mazoezi kila Jumamosi, kwa kuwa hatua hiyo itasaidia kuweka afya za wananchi katika hali bora na nzuri kiafya na hivyo kuwaepusha na magonjwa yasiyotarajiwa.


Wataalamu mbalimbali wa Afya wamekuwa wakihimiza umuhimu wa mazoezi kwa kuwa mazoezi husaidia kuweka mwili wa mwanadamu katika hali nzuri kiafya na hivyo kumsaidia kuondokana na unene uliopitiliza lakini pia kujiepusha na magonjwa kama vile presha ikiwa ni miongoni mwa magonjwa mengine mengi.
BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA BINAGI RADIO
Mbio zikiendelea
Mtaa kwa Mtaa
Mbio zikiendelea
Mazoezi ni mhimu sana
Mazoezi ya Viungo katika Uwanja wa Serengeti Mirongo Jijini Mwanza.
Mazoezi ya Viungo yakiendelea
Hapa watu wa...na...pu...mu..aaaa jeeeee
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu
Ahmed Waziri Gao ambae ni Mwenyekiti wa Timu ya Soka ya Toto Africa ya Jijini Mwanza alikuwa ni miongoni mwa walioshiriki mazoezi hii leo.
Jesca Mbogo nae alishiriki
Neema Deogratius miongoni mwa washiriki 

No comments:

Powered by Blogger.