LIVE STREAM ADS

Header Ads

BINAGI RADIO: NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA AZINDUA MKAKATI WA USAJILI WA WATOTO MKOANI MWANZA.

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh.Ummy Mwalimu (Katikati) akizindua Mkakati wa Usajili wa Watoto walio chini ya Umri wa Miaka Mitano Mkoani Mwanza hii leo uliofanyika katika Ukumbi wa Malaika Hotel Ilemela Mkoani Mwanza.
 Na:George GB Pazzo
Wazazi na Walezi wa Watoto wote walio chini ya Umri wa Miaka Mitano Mkoani Mwanza, wametakiwa kuhakikisha kuwa watoto hao wanasajiliwa na kupatiwa Vyeti vya kuzaliwa.

Rai hiyo imetolewa hii leo na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Ummy Mwalimu, alipokuwa akizindua Mpango wa Kuwasajili Watoto waliochini ya Umri wa Miaka Mitano Mkoani Mwanza, ambao unaoratibiwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini nchini RITA.

Mwalimu amebainisha kuwa Serikali imedhamiria kumsajili na Kumtambua kila mtoto anaezaliwa nchini, na kubainisha kuwa hatua hiyo itaisaidia Serikali katika kuongeza wajibu wake wa kuwahudumia wananchi.

Aidha Mwalimu ametoa rai kwa kwa wasimamizi wa zoezi hilo kuwasajili watoto waliozaliwa Tanzania bara pekee, kwa kuwa Mkakati huo wa Kuwasajili Watoto waliochini ya Umri wa Miaka Mitano umeanza kutekelezwa katika Mikoa ya Tanzania Bara pekee.

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu kutoka RITA Emmy Hudson amebainisha kuwa hakutakuwa na gharama zozote katika Mkakati huo wa Kuwasajili na kuwapatia vyeti vya kuzaliwa watoto walio chini ya Umri wa Miaka Mitano hivyo ni vyema wazazi na walezi wote wakajitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi hilo pindi litakapoanza utekelezaji wake baada ya kuzinduliwa hii leo katika Mkoa wa Mwanza.

Awali akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Manju Msambwa ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Ilemela amebainisha kuwa Mkoa wa Mwanza umeupkea vyema Mkakati huo wa Kuwasajili Watoto walio chini ya Umri wa Miaka mitano ambapo ameahidi kuwa Mkoa wa Mwanza utakuwa mfano bora hata katika Mikoa Mingine katika utekelezaji wa Mkakati huo.

Miongoni mwa Wadau waliofanikisha kuanza kwa utekelezaji wa Mkakati wa Usajili wa Watoto walio Chini ya Umri wa Miaka Mitano na kupatiwa Vyeti vya kuzaliwa ni pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia watoto UNICEF, Kurugugenzi ya Mambo ya nje ya Canada DFTAD, Shirika la Wafanyakazi wa Kujitolea VSO lenye Makao yake Makuu nchini Uingereza na Kampuni ya Mawasiliano nchini ya Tigo ambayo imetoa simu zipatazo 350 zitakazokuwa zikitumika bila gharama kwa ajili ya kusaidia katika zoezi la usajili kwa njia ya Mtandao.


Mkakati wa Kuwasajili watoto walio chini ya Umri wa Miaka Mitano unatumia Teknolojia ya Simu na Kompyuta katika Kutuma na Kutunza kumbukumbu na hivyo kuendana na kasi ya Mabadiliko duniani ambapo tayari umezinduliwa katika Mikoa ya Mbeya, Mwanza na mikoa inayofuata ni Geita, Simiyu pamoja na Katavi na hatimae mikoa mingine yote ya Tanzania Bara.
BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA BINAGI RADIO
Uzinduzi wa Mkakati wa Usajili wa Watoto walio katika chini ya Umri wa Miaka Mitano Mkoani Mwanza. (The Launc of Underfive Birth Registration Initiative in Mwanza Region).
Mh.Ummy Mwalimu akimpokea mmoja wa watoto waliosajiliwa Mkoani Mwanza ikiwa ni katika Uzinduzi wa Mkakati wa Usajili wa Watoto walio chini ya Umri wa Miaka Mitano.
Mh.Ummy Mwalimu Akimpaia Cheti mtoto baada ya usajili hii leo.
Mh.Ummy Mwalimu akijiandaa kumpokea mmoja wa watoto waliosajiliwa Mkoani Mwanza ikiwa ni katika Uzinduzi wa Mkakati wa Usajili wa Watoto walio chini ya Umri wa Miaka Mitano.
Cheti kwa mtoto baada ya usajili
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh.Ummy Mwalimu
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu kutoka RITA Emmy Hudson
Meneja wa Tigo Kanda ya Ziwa Ally Maswanya akizungumza
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela akitoa neno la Shukrani
Viongozi mbalimbali walioalikwa
Washiriki/Viongozi
Viongozi mbalimbali walioshiriki katika Uzinduzi wa Mkakati wa Usajili wa Watoto walio chini ya Umri wa Miaka Mitano Mkoani Mwanza.
Viongozi mbalimbali walioshiriki katika Uzinduzi wa Mkakati wa Usajili wa Watoto walio chini ya Umri wa Miaka Mitano Mkoani Mwanza.
Emmy Hudson kutoka RITA (Kushoto) akiwa pamoja na Mwakilishi kutoka UNICEF
Meza Kuu
Picha ya Pamoja na Mgeni Rasmi Mh.Ummy Mwalimu ambae ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria (wa tano kila upande)
Picha ya Pamoja na Mgeni Rasmi Mh.Ummy Mwalimu ambae ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria (wa tano kila upande)
Meneja wa Tigo Kanda ya Ziwa Ally Maswanya
Meneja wa Tigo Kanda ya Ziwa Ally Maswanya akiongea na wanahabari
Credit:Radio Metro Fm Mwanza
BINAGI MEDIA GROUP PRODUCTIONS

No comments:

Powered by Blogger.