LIVE STREAM ADS

Header Ads

CHAMA CHA MAPINDUZI MKOANI MWANZA CHATOA ONYO KALI JIJINI MWANZA

Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Kushoto) akiwa pamoja na Katibu wa Chama hicho Wilaya ya Nyamagana Elias Mpanda wakiwasili katika Uwanja wa Igogo Kaskazini D Kata ya Igogo Jijini Mwanza hii leo kwa ajili ya Mkutano wa Hadhara ambao umehutubiwa na Mtaturu.
Na:George GB Pazzo
Chama cha Mapinduzi Mkoani Mwanza CCM kimetoa karipio na onyo kali kwa baadhi ya Viongozi wa Kisiasa wanaoshirikiana na wafuasi wao, kushusha na kuchana bendera zake katika maeneo mbalimbali Jijini Mwanza.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu wa Chama hicho Mkoani Mwanza Miraji Mtaturu alipokuwa akiwahutubia wananchi na Makada wa CCM, katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Tawi la Igogo Kaskazini D, Kata ya Igogo Jijini Mwanza.

Mtaturu alibainisha kuwa baadhi ya wanasiasa kwa kushirikiana na Wafuasi wao wamekuwa wakishusha bendera za CCM na kuzichoma huku pia wakiwatishia ama kuwapiga wafuasi wa Chama hicho pindi wanapoonekana katika maeneo mbalimbali wakiwa wamevalia sare za Chama.

Alisema kuwa mwisho wa hayo yote umefika hivyo yeyote atakaethubutu kufanya hivyo na akabainika, ajiandae kupokea adhabu kali atakayokumbana nayo huku akiongeza kuwa chama chochote cha kisiasa kitakachobainika kushusha na kuchana bendera hata moja ya CCM kitakuwa kimeingia katika wakati mgumu kwani adhabu yake itakuwa ni kupoteza bendera 300 ambazo zitakuwa ni mbada wa bendera moja ya CCM.

Kauli ya Mtaturu imejili ikiwa ni siku chache baada ya bendera ya CCM Kushushwa na kuchanwa katika Tawi la Chama hicho la Igogo Kaskazini D, Kata ya Igogo Jijini Mwanza huku ikiwa ni kauli ya pili kutolewa na Mtaturu katika Mikutano yake ya hadhara ambapo kauli kama hiyo aliitoa April 25 mwaka huu alipokuwa akiwahutubia wananchi katika Mkutano wa Hadhara wa Wilaya ya Nyamagana uliofanyika katika Viwanja wa Stand ya Igoma.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtatururu
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza akiwahutubiwa wananchi na WanaCCM katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Kata ya Igogo Jijini Mwanza na kuhudhuriwa na Mamia ya Wananchi.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza akiwahutubiwa wananchi na WanaCCM katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Kata ya Igogo Jijini Mwanza na kuhudhuriwa na Mamia ya Wananchi.
Wananchi na Makada wa CCM wakimsikiliza Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu hii leo katika Uwanja wa Igogo Kaskazini D, Kata ya Igogo Jijini Mwanza.
Wananchi na Makada wa CCM wakimsikiliza Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu hii leo katika Uwanja wa Igogo Kaskazini D, Kata ya Igogo Jijini Mwanza.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula ambae pia ni diwani wa Kata ya Mkolani (CCM) Wilayani Ilemela akitoa salamu zake katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Igogo Jijini Mwanza ambapo Katibu wa CCM Mkoani Mwanza Miraji Mtaturu alikuwa akihuwahutubia wananchi.
Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana Elias Mpanda akitoa salamu zake katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Igogo Jijini Mwanza ambapo Katibu wa CCM Mkoani Mwanza Miraji Mtaturu alikuwa akihuwahutubia wananchi.
Mustapha Banigwa akitoa salamu zake katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Igogo Jijini Mwanza ambapo Katibu wa CCM Mkoani Mwanza Miraji Mtaturu alikuwa akihuwahutubia wananchi.
Kiongozi Chipukizi wa Vijana Wilaya ya Nyamagana (katikati) akisalimia Jukwaani.
Mtoa shairi
Baada ya Shairi umate umate kidogo kutoka Meza kuu
Wakereketwa wa Chama
Maandamano ya WanaIgogo yakiwasili katika eneo la Mkutano
Vijana waliojiunga na CCM Wakisalimiana na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza pamoja na viongozi wengine 
Miongoni mwa waliorudisha kadi ya Chadema
Miongoni mwa waliorudisha kadi ya Chadema akipokea kadi ya CCM
Baadhi ya waliopekea kadi za Chama cha Mapinduzi CCM Wakila kiapo cha Utii
Sehemu ya wananchi na Makada wa CCM Waliohudhuria katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Tawi la Igogo Kaskazini D, Kata ya Igogo Jijini Mwanza ambapo Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu alikuwa akiwahutubia wananchi.
BINAGI MEDIA GROUP PRODUCTIONS

No comments:

Powered by Blogger.