LIVE STREAM ADS

Header Ads

MILIMA YA MAAJABU MKOANI MARA

Hii ni MILIMA ya MAAJABU ambayo inapatikana katika Wilaya ya Rorya mkoani Mara, mita chache kutoka Mto Kirumi ukiwa unatoka au unaelekea Wilayani Tarime ukitokea maeneo mbalimbali katika barabara ya Musoma. 

Maajabu ya hii MILIMA ambayo iko pande zote mbili za barabara si kwamba yanatisha, la hasha. Ni maajabu ambayo ni ya kufurahisha kiukweli hususani ukiwa safarini ambapo ukiitazama utaona namna inavyorudi nyumba na kufanya abiria kuhisi uumbaji wa MUNGU uliotukuka katika hii dunia. 

Ujenzi wa barabara iliyopinda mithiri ya nyoka katika milima hii huifanya kuwa kivutio kingine japo kwa abiria waoga wakifika katika milima hii sara huwa inaongezeka maana si mchezo hususani likija suala la mpando huwa ni mpando kweli, na likija suala la mteremko huwa ni mteremko kweli hivyo kama wewe ni muoga basi huweza hata chungulia nje japo ukweli ni kwamba ukichungulia nje utaona uzuri wa kipekee katika milima hiyo. 

Kikubwa tunaomba shughuli za kibidanamu zisiiathiri milima hii (Tazama picha juu) maana ni tegemea kwa wanamara na sote tunatambua umuhimu wa milima kama hii ambayo ina uwepo mkubwa wa mistu ya asili. 

No comments:

Powered by Blogger.