MKURUGENZI MTENDAJI WA ASMENT AWAFUNGUKIA WAKURUGENZI WA RADIO ZA KIJAMII NCHINI.
Na:Prisca Mshumbuzi
Wamiliki wa Radio za Kijamii
wametakiwa kujenga taswira njema katika Radio hizo ikiwa wanahitaji ziwavutie wasikilizaji wake pamoja na wadau mbalimbaliwa maendeleo hapa nchini.
Rai
hiyo ilitolewa wiki hii Mkoani Mwanza na mwezeshaji wa warsha ya viongozi wa Radio
za Kijamii ambae pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya kuwawezesha wajasiriamali wadogo na
wa kati (ASMET) Ramadhan Ahung.
Ahung
alieleza kuwa malengo ya warsha hiyo na madhumuni yake ni kuwepo kwa mpango wa
biashara ndani ya redio hizo hakutakuwa na maana kama wasipozingatia ujenzi wa
taswira utakaofanywa na wadau kuvutiwa na redio hizo.
“kitu kinachowavutia wasikilizaji ni namna ya kupanga taswira ya Vipindi na namna ya kuvitangaza kwa mvuto ambapo jamii kwa ujumla itavutiwa kuvisikiliza kila siku katika hizi Radio.” Alisema Ahung.
Aidha
Ahung alisema kuwa kuna umuhimu wa Radio za Kijamii pia kuzingatia mahusiano bora
kati yake na wanajamii, watu binafsi pamoja na taasisi za kiraia zenye malengo
tofauti tofauti ambapo alisema hatua hiyo itasaidia radio hizo
kuimarika kibiashara zaidi pia.
“Mahusiano
mazuri ndio msingi wa kuleta maendeleo katika jamii, tofauti na hapo kunaweza kusababisha
marumbano ambayo hayawajengi wanajamii na hivyo mwisho siku Radio za Kijamii
zitaangukia pabaya” Alisema Ahung.
Warsha
hiyo ilikuwa ikihitimisha awamu ya kwanza kwa ufadhili wa mradi wa shirika la
maendeleo la Sweden (SIDA) wa kuzipa uwezo Radio za Kjamii katika matumizi ya
Tehama chini ya uratibu wa shirika la kimataifa la elimu sayansi na utamaduni
UNESCO iliyofanyika katika kituo cha Radio Sengerema Mkoani Mwanza.
No comments: