UMOJA WA ULAYA KUENDELEA KUIKOMALIA SERIKALI YA TANZANIA.
Meza kuu katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari
Duniani. Kutoka kushoto ni Makamu wa
Rais wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa Habari nchini (UTPC), Jane Mihanji,
Mkurugenzi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Bw. Ernest Sungura,
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi na Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez.
Na:Edwin Soko
Jumuiya ya nchi za Ulaya imesema kuwa itaendelea kupaza sauti yake kwa serikali ya Tanzania katika kulinda na kuheshimu haki za binadamu, ikiwemo uhuru wa vyombo vya habari pamoja na haki ya kupata habari ili kuchochea kukua kwa maendelea ya kidemokrasia Nchini.
Hayo yalisemwa na balozi wa umoja wa ulaya Nchini Tanzania Filibero Ceriansebregondi alipokuwa anafungua rasmi kilele cha maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani kwa mwaka huu yaliyofanyika Mkoani Morogoro.
Ceriansebregondi alibainisha kuwa uwakilishi wake Nchini Tanzania utalenga kufanya mashauriano na serikali juu ya kuheshimu uhuru wa vyombo vya habari na haki ya kupata habari kwa kuwa ni nguzo muhimu kwa Nchi yoyote katika kupata maendeleo popote duniani.
Naye mratibu wa umoja wa ulaya Tanzania Alvero Rodriguez alisema kuwa, huu ni mwaka muhimu sana kwa Tanzania na jumuiya za kimataifa, kuhakikisha nafasi ya waandishi wa habari inapewa thamani yake hususani katika shughuli za uchaguzi mkuu.
Rudriguez alibainisha kuwa jukumu hilo kwa waandishi lazima lifuate maadili ya uandishi wa habari kwa kuhakikisha kuwa haki na usawa pamoja na ulinganifu wa habari unazingatiwa, pamoja na watawala kutoweka sheria nyingi zenye kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari.
Naye mwenyekiti wa wa taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa jangwa la Sahara Saimon Berege alisema kuwa Tanzania imeporomoka katika viwango vya kimataifa vya kulinda na kuheshimu uhuru wa vyombo vya habari.
Berege alisema kuwa, kwa mujibu wa taasisi ya waandishi wa habari wasio na mipaka Tanzania imeshika nafasi ya 75 duniani kwa kuheshimu uhuru wa vyombo vya habari hadi kufikia mwezi April, 2015 toka nafasi ya 69 kwa mwaka 2014.
Barege alisistiza kuwa hiyo yote inatokana na uwepo wa mazingira mabaya ya kulinda uhuru wa vyombo vya habari hapa Nchini ikiwemo kutungwa kwa sheria mbaya na kandamizi kwa vyombo vya habari, vitisho na vipigo kwa baadhi ya waandishi.
Pia alisisitiza kuwa, inasikitisha kuona Nchi yenye magazeti zaidi ya 800 redio zaidi ya 100 lakini Nchi hiyo hiyo inatunga sheria mbaya zenye kukandamiza vyombo vya habari.
Kwa upande wake wenyekiti wa jukwaa la wahariri Tanzania Absalom Kibanda alisema kuwa, kimsingi maadhimisho ya mwaka huu yanahitimisha miaka 10 ya unyanyaswaji wa tasnia ya habari kuliko awamu zote za uongozi zilizopita, kwani serikali inayomaliza muda wake ndiyo iliyokiuka kwa kiasi kikubwa uhuru wa vyombo vya habari, kwa kuuawa kwa mwanahabari Daud Mwangozi, kujeruhiwa kwa baadhi ya waandishi wa Habari na kutungwa kwa sheria mbaya na kandamizi ikiwemo sheria ya takwimu na makosa ya mtandanioni.
Maadhimisho hayo yalienda sanjari na mada mbalimbali na kufuatiwa na ushuhuda wa waaandishi wa habari waliowahi kupata maswahibu katika tasnia ya habari , akiwemo Josephat Isango aliyekuwa mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima, Maxence Melo mmiliki wa mtandao na jamii forum na Majjid Mjengwa mmiliki wa blog ya mjenjwa .
Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani kilifanyika May Mbili ambapo Kauli mbiu yake ilikuwa inalenga juu ya Usalama wa Habari katika dhama za Dijitali, uandishi bora, usawa wa kijinsia na faragha.
No comments: