LIVE STREAM ADS

Header Ads

"MSIWACHAGUE VIONGOZI WAZEMBE KAMA HUYU". ASEMA KATIBU WA CCM MKOA WA MWANZA.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoani Mwanza Miraji Mtaturu (wa kwanza Kushoto) pamoja na viongozi wengine wa chama, akipita jana katika eneo la Bugarika Sokoni Kata ya Pamba Jijini Mwanza ambapo kulikuwa na Kilele cha Wiki ya Jujuiya ya Wazazi wa CCM Kimkoa. 
Pembeni linaonekana eneo la kukusanyia Uchafu ambapo uchafu katika eneo hilo umefurika na Kuzagaa ovyo kiasi cha kuhatarisha wananchi wa Bugarika wanaotegemea Soko lililopo katika eneo hilo. Kutokana na Uchafu kuleta kero katika eneo hilo, Mtaturu alitoa siku nne uchafu huo uwe umeondolewa haraka iwezekanavyo na kuahidi kwenda kukagua eneo hilo siku ya alhamisi ya ijayo May Sita.
Alisema atafuatili ili kujua ni kwa nini uchafu katika eneo hilo haundolewi na kama kuna Mzabuni mwenye hiyo tenda, basi atahakikisha anawajibishwa kutokana na kushindwa kutimiza majukumu yake ipasavyo. Aidha alitoa changamoto kwa Diwani wa Kata ya Pamba Samwel Range kutokana na kukaa kimya huku akijionea hali ilivyo mbaya katika eneo hilo la Bugarika Sokoni ambapo aliwasihi wananchi kutofanya makosa tena kwa kuwachagua viongozi wazembe mithili ya diwani huyo ambae anatoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema.
 Na:George GB Pazzo
Katibu wa CCM Mkoani akijioneahali ilivyo tete katika dampo la Bugarika Sokoni Jijini Mwanza baada ya uchagu kujaa na kuzagaa ovyo katika eneo hilo, tena katika kipindi cha Mvua, ni zaidi ya Hatari.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (mwenye miwani) akielekea katika Shule ya Sekondari Bugarika kwa ajili ya zoezi la upandaji wa Miti ikiwa ni katika Kuadhimisha Kilele cha Wiki ya Jumuiya ya Wazazi nchini ambayo Kimkoa katika Mkoa wa Mwanza ilifanyika jana.
Tunza Mazingira, yakutunze...Vijana wa Chama cha Mapinduzi wakiendelea na zoezi la Upandaji Miti katika eneo la Zahanati ya Bugarika Jijini Mwanza. Zahanati hii hutoa huduma za Uzazi wa Mama na Mtoto.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akishiriki zoezi la kupanda miti katika eneo la Zahanati ya Bugarika Jijini Mwanza ikiwa ni katika Kuadhimisha Kilele cha Wiki ya Jumuiya ya Wazazi nchini ambayo Kimkoa katika Mkoa wa Mwanza ilifanyika jana
Dinah Samani (alieinama) ambae ni Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Mwanza akipanda mche katika eneo la Zahanati ya Bugarika ikiwa ni katika Kuadhimisha Kilele cha Wiki ya Jumuiya ya Wazazi nchini ambayo Kimkoa katika Mkoa wa Mwanza ilifanyika jana
Anna Sulley (alieinama) ambae ni Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza akipanda mche katika eneo la Zahanati ya Bugarika ikiwa ni katika Kuadhimisha Kilele cha Wiki ya Jumuiya ya Wazazi nchini ambayo Kimkoa katika Mkoa wa Mwanza ilifanyika jana
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza akipanda mche katika eneo la Zahanati ya Bugarika ikiwa ni katika Kuadhimisha Kilele cha Wiki ya Jumuiya ya Wazazi nchini ambayo Kimkoa katika Mkoa wa Mwanza ilifanyika jana
Mwanahabari Fredirick Katulaka kutoka Gazeti na Radio Uhuru akipanda mche katika eneo la Zahanati ya Bugarika ikiwa ni katika Kuadhimisha Kilele cha Wiki ya Jumuiya ya Wazazi nchini ambayo Kimkoa katika Mkoa wa Mwanza ilifanyika jana
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (mwenye kofia) pamoja na Viongozi wengine wa Chama wakiondoka baada ya kupanda Miche katika Shule ya Bugarika Sekondari.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Elias Mpanda (Katikati) akiwa na wakereketwa watarajiwa wa Chama hicho.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akiwasili katika eneo la Bugarika Kaskazini kwa ajili ya Kuzindua Shina la Vijana Wakereketwa wa Chama hicho lenye wanachama 30. Katika Shina hilo Mtaturu alliwasihi vijana kuendelea kujiunga katika Vikundi ili kuendelea kunufaika na Fursa zinazotolewa kwa ajili yao. Aliweza kuwachangia Shilingi Milioni Moja kwa ajili ya kuimarisha shughuli zao pamoja kuahidi kuwaandalia Semna elekezi ili waweze kufundishwa zaidi masuala ya Ujasiriamali.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Nyamagana Anna Sulley (mwenye kinasa sauti) akizungumza mapema kabla Katibu wa CCM Mkoani Mwanza Miraji Mtaturu (katikati) hajazindua tawi la Wakereketwa wa Chama hicho Tawi la Bugarika Kaskazini.
Risala kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza ikisomwa
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Wa Pili kushoto) akizindua Tawi la Wakereketwa wa CCM Tawi la Bugarika Kaskazini Kata ya Pamba Jijini Mwanza.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akipandisha bendera ya chama hicho baada ya kuzindua Tawi la Wakereketwa wa CCM Bugarika Kaskazini.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akizungumza baada ya Kuzindua Tawi la Wakereketwa wa CCM Tawi la Bugarika Kaskazini Kata ya Pamba Jijini Mwanza siku ya jana.
Bango linasomeka vyema
Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Elias Mpanda (alieshika kinasa sauti) akimkaribisha Dinah Samani ambae ni Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoani Mwanza (anaepanda ngazi) ili kusoma Risara ya Jumuiya hiyo ikiwa ni katika Kilele cha Wiki ya Wazazi nchini ambayo Katika Mkoa wa Mwanza ilifanyika jana May 02, 2015 katika Viwanja vya Bugarika Sokoni Kata ya Pamba Jijini Mwanza.
Jukwaan ni Dinah Samani ambae ni Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoani Mwanza akizungumza katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Bugarika Sokoni Jijini Mwanza ikiwa ni katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Wazazi nchini ambapo katika Kimkoa Mkoani Mwanza ilifanyika jana.
Charles Nyamasiriri (mwenye kinasa sauti) ambae ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza akitoa salamu zake jana katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Bugarika Sokoni Jijini Mwanza ikiwa ni katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Wazazi nchini ambapo katika Kimkoa Mkoani Mwanza ilifanyika jana.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akiwahutubia wananchi katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Bugarika Jijini Mwanza. Mtaturu alikuwa Mgeni Rasmi katika Kilele cha Wiki ya Wazazi nchini ambayo Katika Mkoa wa Mwanza ilikuwa jana katika Viwanja vya Bugarika Jijini Mwanza.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akiwahutubia wananchi katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Bugarika Sokoni Jijini Mwanza ikiwa ni katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Wazazi nchini ambapo katika Kimkoa Mkoani Mwanza ilifanyika jana.
Zaidi ya wanachama 120 wapya walijiunga na Chama cha Mapinduzi CCM na hapa wakisalimiana na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza pamoja na viongozi wengine wa Chama baada ya kupokea kadi za uanachama.
Zaidi ya wanachama 120 wapya walijiunga na Chama cha Mapinduzi CCM na hapa wakisalimiana na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza na viongozi wengine wa Chama baada ya kupokea kadi za uanachama.
Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Elias Mpanda (Kushoto) akiwaapisha wanachama wapya zaidi ya 120 waliojiunga na CCM jana na kupatiwa kadi za uanachama.
Wanachama wapya zaidi ya 120 wakipokea kiapo baada ya kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM
Burudani ilikuwa tamu sana.
Makada wa CCM pamoja na wananchi wakifuatilia matukio
Makada na Viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Mwanza.
Credit:Radio Metro

No comments:

Powered by Blogger.