LIVE STREAM ADS

Header Ads

BEST NASSO AWEKA HISTORIA NDANI YA MARSH HOTEL JIJINI MWANZA.

Katika kusherekea Shangwe za Siku ya Wafanyakazi Duniani Maarufu kwa jina la Mei Mosi iliyoadhimishwa Ijumaa iliyopita ya tarehe 01:05.2015, Msanii Best Nasso kutoka Mkoani Mara aliweza kuandika historia Moja Matata baada ya kudondosha Burudani ya nguvu kwa wakazi wa Jiji la Mwanza na Viunga Vyake. Burudani hiyo ilipigwa katika Kiota cha Burudani cha MARSH HOTE kilichopo Nyakato National Jijini Mwanza.
Pamoja na Kwanza viota vingi jijini Mwanza vilikuwa vikitoa burudani za aina mbalimbali, lakini kwa Upande wa Marsh Hotel burudani ilikuwa ya kuvutia sana, hadi wapenda burudani waliokuwepo Hotelini hapo wakaomba kuwepo kwa mwendelezo wa burudani katika kiota hicho mara kwa mara, ombi ambalo lilikubaliwa na Uongozi wa Marsh Hotel.
TAZAMA PICHA ILIVYOKUWA.
Na GB Pazzo
Msanii Best Nasso akiwajibika Jukwaani katika Kiota cha burudani kilichopo Marsh Hotel Jijini Mwanza
Tugei tano Nasso
"Hadija weee...Hadija Mama...hahahahahaaaaaa Nasso bwana alipiga show ya maana sana.
"Hapa Best Nasso akiimba wimbo unaojulikana kwa jina la Nipe Nafasi....Watu wanapenda sana huo wimbo.
Hatimae wapenda burudani uvumilivu ukawashinda na hivyo huyu dada akapanda jukwaani kucheza na Best Nasso
Mwingine nae tena akisakata ngoma na Best Nasso
Miongoni mwa washereheshaji akiwajibika jukwaani
Huyu Mshikaji anaitwa KIDMASE, kiukweli katika ngoma za Reggae alibaba sana
Wapenda burudani wakisakata ngoma
Palikuwa hapatoshi....ilikuwa ni mwendo wa kusakata ngoma
Hatimae wapenda burudani wakaanza kuweka Kumbukumbu na Kamera ya Binagi Media Group
Washereheshaji a.k.a Ma-Mc wakaweka kumbukumbu na Kamera ya Binagi Media Group
Na hawa washkaji nao walikuwepo
Mc bwana kaka Mzee wa Kifimbo cheza Vile...Yeye na Mkongojo hadi jukwaani
Kumbukumbu ziliendelea katika Kamera ya Biagi Media Group
Hapa Best Nasso (Wa pili kushoto) akiwa na Matajiri wa Jiji la Mwanza kwa ajili ya Kushow Love na Kamera ya Binagi Media Group.
Matajiri wa Jiji la Mwanza wakishow Love na Kamera ya Binagi Media Group.
Chimbuko la Burudani a.k.a Sound lilikua likichomoza kutoka hapa
Msanii Best Nasso (Wa pili Kulia) akiwa na Matajiri wengine wa Mwanza wakishow Love na Kamera ya Binagi Media Group. Ilikuwa hivyo katika Usiku wa MEI MOSI ndani ya MARSH HOTEL JIJINI MWANZA ambapo Msanii BEST NASSO alikinukisha mbaya.
ENDELEA KUTEMBELEA BINAGI MEDIA GROUP AMBAPO TUTAKUWA TUKIKULETEA TAARIFA ZA BURUDANI ZITAKAZOKUWA ZIKIANDALIWA KWA AJILI YAKO NDANI YA MARSH HOTEL JIJINI MWANZA.
BINAGI MEDIA GROUP PRODUCTIONS

No comments:

Powered by Blogger.