LIVE STREAM ADS

Header Ads

SERIKALI YA MISRI YASHUSHA KONTENA LA VIFAA KATIKA HOSPITAL YA JESHI LA POLISI KILWA ROAD DAR.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya kontena lenye vifaa vya chumba cha kuhifadhia maiti vilivyotolewa na Serikali ya Misri katika Hospitali ya Jeshi la Polisi nchini Kilwa Road Jijini Dar es Salaam jana.
PICHA ZOTE NA ABUBAKARI AKIDA- WIZARA YA MAMBO YA NDANI
Balozi wa Misri Nchini, Hossam Moharam (kulia), akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kushoto), kontena lenye vifaa vya chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Jeshi la Polisi Kilwa Road. Wa kwanza kushoto ni Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Abdulrahmani Kaniki.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kushoto), akiongozana na Balozi wa Misri Nchini, Hossam Moharam (kulia), kuelekea kwenye jengo litakalotumika kwa ajili ya kuhifadhia maiti katika hospitali ya Jeshi la Polisi Kilwa Road jijini Dar es Salaam.
Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Abdulrahman Kaniki akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya kontena lenye vifaa vya chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Jeshi la Polisi Kilwa Road jijini Dar es Salaam.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi nchini, Richard Malika akitoa maelezo kuhusu mchoro wa jengo la kuhifadhia maiti linalojengwa katika Hospitali ya Jeshi la Polisi Kilwa Road jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi na Balozi wa Misri Nchini, Hossam Moharam wakimsikiliza.

No comments:

Powered by Blogger.