SERIKALI YATAKIWA KUSAIDIA MAPAMBANO DHIDI YA MAAMBUKIZI YA MAGONJWA YA SARATANI.
Washiriki wa Semna ya Uhamasishaji Viongozi wa Afya Mkoani Mwanza kuhusu kupambana na Ugonjwa wa Saratani ya Shingo ya Kizazi wakiwa katika Mafunzo kwa Vitendo mwishoni mwa mwaka jana.
MALONGO MBEHO
Serikali imetakiwa kuendelea kuwawezesha wadau mbalimbali
wa afya hapa nchini ili kusaidia katika mapambano dhidi ya maambukizi ya magonjwa ya
Saratani.
Hayo yalisemwa jana na Dr.Amina
Jumanne Yusuph ambae ni daktari wa magonjwa ya saratani ya shingo ya kizazi kwa
akina mama kutoka Hospitali ya Rufaa Bugando wakati akizungumza na Radio
Metro Jijini Mwanza.
Dr.Yusuph alisema kuwa bado maambukizi
ya Saratani ya Shingo ya Kizazi kwa akina mama hapa nchini yapo juu huku Mikoa
ya Kanda ya Ziwa ikiwa katika kiwango kikubwa zaidi cha maambukizi hayo.
Akieleza sababu za Maambukizi hayo kuwa
katika kiwango kikubwa hususani katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa, Dr.Yusuph
alisema kuwa hiyo inatokana na ushiriki wa ngono zembe katika maeneo ya uzalishaji maeneo ya Migodini na Visiwani katika kambi za wavuvi.
Alibainisha kuwa Maambukizi hayo huambukizwa kwa njia ya Kujamiana hivyo maambukizi hayo kwa
njia ya zinaa yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku hadi kufikia takribani asilimia 99 hapa
nchini.
"Serikali iendelea kuwawezesha
wahudumu wa afya ili kuendelea kutoa elimu katika jamii kwa lengo la kupambana
na Maambukizi ya Saratani ya Shingo ya Kizazi kwa wanawake maana maambukizi haya hugharimu maisha ya wanawake wengi". Alisema Dr.Yusuph na kuongeza;
“Wanajamii
pia wanatakiwa kujijengea tabia ya kupima afya zao mara kwa mara kwani Vipimo vya saratani
ya shingo ya kizazi hutolewa bila malipo katika hospitali mbalimbali ikiwemo
Hospitali ya Rufaa Bugando”.
Inaelezwa kuwa zaidi ya wanawake elfu thelathini na tano kwa mwaka hupoteza maisha hii ikiwa ni kwa kila maambukizi laki moja yanayotokea.
No comments: