SERIKALI YAKIRI KUSHINDWA KUFIKIA MALENGO ILIYOJIWEKEA.
ELISA ANATORY
EMAIL anatoryelisa@gmail.com
Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeshindwa
kufikia lengo namba tano la maendeleo la milenia katika kuboresha afya ya uzazi
kwa mwaka 2015 hivyo inajipanga upya ili kufikia upya malengo hayo hadi kufikia
mwaka 2020.
Hayo
yalisemwa jana bungeni Mjini Dodoma na naibu waziri wa habari, vijana, utamaduni
na michezo Juma Nkamia kwa niaba ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr.Seif
Rashid wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalum Anastazia Wambura aliyetaka kujua mikakati ya serikali
juu ya malengo ya milenia kuhusu kuboresha afya ya uzazi nchini.
Waziri
Nkamia alisema kuwa lengo namba tano la malengo ya milenia lilikuwa ni kupunguza
vifo vya wanawake na watoto vitokanavyo na uzazi kutoka vifo 529 kwa kila
vizazi hai laki moja hadi kufikia chini ya vifo 193 kwa vizazi hai laki moja.
“Japokuwa
malengo yaliyowekwa hayajafikiwa lakini juhudi za mpango huo zimezaa matunda
ambapo takwimu za sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 zinaonyesha kuwa vifo
vitokanavyo na uzazi vimeshuka hadi kufikia vifo 432 kwa vizazi hai laki moja”.
Alisema Nkamia na kuongeza kuwa Serikali inafanya kila jitihada ili kufikia malengo
ya Milenia iliyojiwekea hadi kufikia mwaka 2010.
No comments: