LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAMBUA UWEPO WA SOPHIA NA GB PAZZO NDANI YA RADIO METRO FM YA JIJINI MWANZA.

Sophia George (Kushoto) ambae ni Mtangazaji wa Radio Metro, Pamoja na Wewe ya Jijini Mwanza akiwa pamoja na George GB Pazzo (Kulia) ambae pia nae ni Mtangazaji na Mwandishi wa Habari wa Radio hiyo huku pia akiwa ndie C.E.O wa Binagi Media Group, Kwa Pamoja Tuijuze Jamii.

Sophia anasikika katika Kipindi cha Mambo Mtelezo Kila Siku za Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa Tatu Kamili asubuhi hadi saa Saba Kamili Mchana akiwa pamoja na Amina Rashid Pamoja na Barazeduka Anselimo lakini pia anasikika katika Kipindi cha Vidole Juu kila siku ya Jumapili kuanzia saa Kumi Kamili Alasiri hadi saa mbili kamili usiku akiwa pamoja na Amina Rashid.

GB Pazzo utakutana nae katika Kipindi cha Metro Evening Drive kila siku za Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa Kumi alasiri hadi saa Kumi na Mbili na nusu jioni akiwa pamoja na Sefroza Joseph, Malongo Mbeho, Julieth Kashaigili lakini pia utakuwa nae kila siku ya Jumamosi kuanzia saa Nne Kamili Usiku hadi saa Sita Kamili Usiku ndani ya Saturday Club Mixing kwa ajili ya Milipuko ya burudazi za Wikend!
Leo Binagi Media Group imekuletea uwepo wa Watangazaji hao hivyo usikose Kuisikiliza 99.4 Radio Metro Fm, Pamoja na Wewe kila siku ili kuburudika na kuhabarika zadi.
Sophia George (Kushoto) ambae ni Mtangazaji wa Radio Metro Fm ya Jijini Mwanza akiwa pamoja na GB Pazzo (Kulia) @Metro Fm & C.E.O @Binagi Media Group.
GB Pazzo (Kulia) @Metro Fm & C.E.O @Binagi Media Group akiwa pamoja na Sophia George @Metro Fm (Kushoto).
GB Pazzo @Metro Fm & C.E.O @Binagi Media Group

No comments:

Powered by Blogger.