LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAHAFALI YA TATU YA KIDATO CHA SITA KATIKA SHULE YA SEKONDARI MKOLANI JIJINI MWANZA YAFANA.

Wanafunzi wahitimu wa Kidato cha Sita kutoka Shule ya Sekondari Mkolani iliyopo Jijini Mwanza, wakiwa katika Picha ya Pamoja na Mgeni Rasmi Raphael Shiratu (Wa tatu kushoto waliokaa) ambae ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza. Shilatu pia ni Meneja Utumishi na Utawala katika Kampuni ya Sahara Media Group.
Hii Ilikuwa leo Ijumaa May 15, 2015 katika Mahafari ya Wanafunzi hao yalifanyika katika Ukumbi wa Shule hiyo ambapo Shilatu alikuwa Mgeni Rasmi. Wengine wanaoonekana ni Mkuu wa Shule hiyo pamoja na baadhi ya Wageni Waalikwa waliohudhuria katika Mahafali hayo ambayo ni ya tatu tangu shule hiyo ya Mkolani ianze kupokea wanafunzi wa Kidato Chano na Sita.

Jumla ya Wanafunzi 53 ambapo wa Kike ni 48 na wa Kiume Watano ambao walijiunga na Kidato cha Tano Mwezi July mwaka 2013 katika Shule ya Sekondari Mkolani iliyopo Kata ya Mkolani Jijini Mwanza wameweza kuhitimu masomo yao ya Kidato cha Sita. Wanafunzi hao walikuwa katika Michepuo ya PCM, PCB pamoja na CBG.
Na:George GB Pazzo
Mgeni Rasmi katika Mahafali ya Tatu ya Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari Mkolani iliyoipo Jijini Mwanza Raphael Shilatu (Wa tatu kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya Pamoja na baadhi ya wageni waalikwa, Mkuu wa Shule pamoja na Waalimu wa Shule hiyo.
Wahitimu wa Kidato cha Sita Mkolani Sekondari wakiingia Ukumbini hii leo ikiwa ni katika Sherehe za Mahafali ya Tati ya Kidato cha Sita shuleni hapo.
Wahitimu wa Kidato cha Sita Mkolani Sekondari ya Jijini Mwanza wakiingia Ukumbini ikiwa ni katika Sherehe za kusherehekea Mahafali ya Tatu ya Kidato cha Sita ya Shule hiyo.
Wahitimu wa Kidato cha Sita Mkolani Sekondari iliyopo Jijini Mwanza wakijibwaga Ukumbini katika Kusherehekea Mahafari yao hii leo.
Wahitimu wa Kidato cha Sita Mkolani Sekondari iliyopo Jijini Mwanza
Wahitimu wa Kidato wa Sita Mkolani Sekondari ilyopo Jijini Mwanza
Miongoni mwa wahitimu wa Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari Mkolani iliyopo Jijini Mwanza.
Wahitimu wa Kidato cha Sita Mkolani Sekondari iliyopo Jijini Mwanza wakiwa katika Mahafali yao yaliyofanyika hii leo katika Ukumbi wa Shule hiyo iliyopo Kata ya Mkolani.
Miongoni mwa Wahitimu akibonga na Kinasa sauti cha Radio Metro Fm ya Jijini Mwanza.
Miongoni mwa wahitimu wa Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mkolani akibonga na Kinasa sauti cha Radio Metro ya Jijini Mwanza
Wanafunzi wa Mkolani Sekondari wanaobaki
Meza Kuu
Walioketi mbele ni Redempta Majigwa (Kushoto) ambae ni Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza, katikati ni Esther Mchalundi ambae ni Mwenyeki wa UWT Kata ya Mkolani Wilaya ya Nyamagana na anaefuata ni Raphael Shilatu (kulia) ambae ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza. Shilatu pia ni Meneja Utumishi na Utawala katika Kampuni ya Sahara Media Group.
Walioketi nyuma ni waalimu wa Mkolani Sekondari.
Kushoto ni Anna Ruhumbika ambae ni Mwalimu wa Taaluma Mkoani Sekondari akifuatiwa na Haindo Ngowi ambae ni Mratibu wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Jijini Mwanza TASAF.
Haindo Ngowi ambae ni Mratibu wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Jijini Mwanza TASAF.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Mkolani Asensio Mathias akizungumza katika Mahafali ya Tatu ya Kidato cha Sita ya Shule hiyo yaliyofanyika hii leo katika Ukumbi wa Shule hiyo.
Raphael Shilatu ambae ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nyamagana akizungumza katika Mahafali ya Tatu ya Kidato cha Sita ya Shule ya Sekondari Mkolani iliyopo Jijini Mwanza yaliyofanyika hii leo katika Ukumbi wa Shule hiyo. Shilatua alikuwa Mgeni Rasmi katika Mahafali hayo. Shilatu amechangia Mifuko 10 ya Theluji kwa ajili ya Kusaidia Ujenzi wa darasa linalotarajiwa kujengwa katika Shule hiyo kwa nguvu za wananchi.
Alijitambulisha kwa jina la Sauti nyororo ambapo hapa alikuwa akitoa salamu kwa niaba ya wazazi katika Mahafali ya Tatu ya Kidato cha Sita Mkolani Sekondari.
Wanafunzi wenye Mahitaji Maalumu wanaosoma katika Shule ya Sekondari Mkolani iliyopo Jijini Mwanza wakitoa burudani ya nyimbo katika Mahafali ya Tatu ya Kidato cha Sita katika Shule hiyo yaliyofanyika hii leo katika Ukumbi wa Shule hiyo.
Mgeni Rasmi katika Mahafali ya Tatu ya Kidato cha Sita katika shule ya Sekondari Mkolani iliyopo Jijini Mwanza Raphael Shilatu akiwakabidhi wanafunzi wenye mahitaji maalumu wanaosoma shuleni hapo Fedha kiasi cha Shilingi Laki Moja na Elfu Thelani na Tano (135,000) alizozichanga kwa kushirikiana na wageni waalikwa, waalimu na wanafunzi kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi hao katika mahitaji yao. Aliesimama kushoto ni mwalimu wa wanafunzi hao wa Lugha ya ishara (Kwa wasiosikia),
Mkuu wa Shule ya Sekondari Mkolani akipokea fedha zilizochangishwa na Shilatu kutoka kwa mmoja wa wanafunzi wenye mahitaji maalumu wanaosoma shuleni hapo.
Ashura Suleman (Kushoto) akisoma Risala ya wahitimu wa Tatu ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mkolani iliyopo Jijini Mwanza. Kulia ni Zephania Elias.
Mmoja wa wahitimu wa Kidato cha Sita Mkolani Sekondari akipokea Cheti
Miongoni mwa wahitimu wa Kidato cha Sita Mkolani Sekondari akipokea Cheti
Mhitimu wa Kidato cha Sita Mkolani Sekondari akipokea Cheti
Meza kuu ambapo aliketi Mgeni Rasmi, Waalimu wa Mkolani Sekondari pamoja na wageni waalikwa.
Baadhi ya Waalimu wa Mkolani Sekondari ya Jijini Mwanza
Miongoni mwa waalimu wa Mkolani Sekondari iliyopo Jijini Mwanza.
Na
BINAGI MEDIA GROUP, KWA PAMOJA TUIJUZE JAMII-0757 43 26 94

No comments:

Powered by Blogger.