LIVE STREAM ADS

Header Ads

WENYEVITI UKAWA WAGOMEA KIKAO CHA MAENDELEO JIJINI MWANZA NA KUSABABISHA KIKAO KUVUNJIKA.

John Minja (Aliesimama).
Na:Genya Richard
Kikao cha Maendeleo cha Kata ya Igogo Jijini Mwanza Kimeshindwa Kuendelea baada ya Wenyeviti wa Serikali za Mitaa katika Kata hiyo wanaotokana na Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA kugomea kikao Hicho.

Kikao hicho kilichokuwa kimeketi jana katika Ofisi ya Kata hiyo ya Igogo, kilivunjika baada ya wenyeviti wanaotoka katika Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi Ukawa, kudai kuwa kilikuwa ni kikao batili na hakina agenda na hivyo kumtaka mwenyekiti kukiahirisha hadi wakati mwingine kitakapoketi kikiwa na agenda toshelezi.
“…Mwenyekiti unaahirisha kikao au unataka tufanye vurugu, Maana unatupelekesha unavyotaka wewe…Kwanza kikao hakina agenda zinazoeleweka…”.Walisikika wakisema wenyeviti wa Mitaa ya Malulu, Bugando na mingineyo ambao wanatokana na Vyama vya Ukawa huku wakisimama na kutoka nje ya Ukumbi.

Mwenyekiti wa Kikao hicho John Austino Minja ambae ni Diwani wa Kata ya Igogo (CCM) na Naibu Meya wa Jiji la Mwanza alieleza kusikitishwa kwake kwa hatua ya kikao hicho kuvurugika huku akibainisha kuwa lengo lake lilikuwa ni kujadili mipango ya Maendeleo ya Kata hiyo kwa ajili ya maboresho na kufanikisha kwa wakati ujenzi wa Maabara katika shule za Sekondari Katani hapo.

No comments:

Powered by Blogger.