LIVE STREAM ADS

Header Ads

ILIVYOKUWA KATIKA ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM WILAYANI ILEMELA MKOA WA MWANZA HII LEO.

Msafara wa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndg.Abdulrahman Kinana (Wa tatu kutoka Kulia) ukielekea katika Ukumbi wa Chuo cha Mali Asili Pasiansi Wilayani Ilemela hii leo kwa ajili ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilayani humo.
Awali kabla ya Mkutano huo, Kinana alizindua Mashina Mawili ya Vijana Wakereketwa wa CCM ambayo ni UVCC Gogo Vinu lililopo Kona ya Bwiru pamoja na UVCCM Upendo lililopo Pasiansi.
Baada ya shughuli hizo Kinana alipata fursa ya Kukagua Mradi wa Maji wa Sangabuye, Ujenzi wa Zahanati ya Monze iliyopo Kata ya Bugogwa ambapo ameahidi kusaidia ujenzi huo kwa kutoa Mifuko 50 ya Theluji na hatimae aliweza kukutana na Wananchi wa Bwilu na kusikiliza kero zao za hususani za Migogoro ya ardhi ambapo aliahidi kuifikisha ngazi zinazohusika Migogoro hiyo kwa ajili ya Utatuzi.
Na:George GB Pazzo
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndg.Abdulrahman Kinana akipandisha bendera ya Chama baada ya Uzinduzi wa Shina la Vijana Wakereketwa wa CCM la UVCCM Upendo lililopo Pasiansi Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndg.Abdulrahman Kinana (Kulia) akipokea taarifa ya ujenzi wa mradi wa chanzo cha Maji Sangabuye Wilayani Ilemela.
Msafara wa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndg.Abdulrahman Kinana ukijionea ujenzi wa Mashine za kusukuma maji zilizopo katika mradi wa Maji wa Sangabuye Wilayani Ilemela.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Ndg.Abdulrahman Kinana akizungumza na Wananchi wa Bwilu hii leo alipifika kwa ajili ya kusikiliza kero zao zinazowakabiri hususani kero za ardhi zinazolalamikiwa kwa muda mrefu na wananchi hao.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Ndg.Abdulrahman Kinana (Kushoto) akiwa pamoja na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Kulia).
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo akitoa ufafanuzi wa Malalamiko ya Wananchi wa Bwilu wanaolalamika kupokwa ardhi yao wakati Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Ndg.Abdulrahman Kinana alipofika kusikiliza kero za wananchi hao.
Mmoja wa Wananchi wa Bwilu Wilayani Ilemela akitoa Malalamiko yake kwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana ambae alifika Katani hapo hii leo ili kusikiliza kero zinazowakabiri.
Mmoja wa Wananchi wa Bwilu Wilayani Ilemela akitoa Malalamiko yake kwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana ambae alifika Katani hapo hii leo ili kusikiliza kero zinazowakabiri.
Wananchi wa Kata ya Bwilu Wilayani Ilemela waliokusanyika hii leo ili kuwasilisha Malalamiko yao ya kupokwa ardhi yao kwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana ambae alifika Katani hapo hii leo ili kusikiliza kero zinazowakabiri.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM ngazi ya Taifa Nnape Nhauye akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana wakati wa Uzinduzi wa jengo la Chama cha Madereva wa Malori Buswelu Wilayani Ilemela hii leo.
Juma Mzungu (Kushoto) ambae ni Katibu wa Chama cha Madereva wa Malori Buswelu akisoma Risala ya Chama
Umoja wa Wa Waendesha Pikipiki pia nao Ulipata nafasi ya Kuwasilisha Risala yao kwa Ndugu Nnape Nhauye ambae aliwaahidi kuwasaidia kupata Mikopo ya Pikipiki kwa riba nafuu ili wanachama wa umoja huo waweze kumiliki pikipiki zao wenyewe. Pia amesaidia kuwachangia fedha kwa ajili ya Ujenzi wa Ofisi ya Umoja huo.
Afisa Ardhi Wilaya ya Ilemela akitoa mikakati iliyopangwa na Manispaa ya Ilemela ili kupata eneo kwa ajili ya Shughuli ya Uchimbaji wa Mchanga katika eneo la Buswelu
Viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoani Mwanza wakiongozwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Wa kwanza Kushoto).

No comments:

Powered by Blogger.