LIVE STREAM ADS

Header Ads

JB BELMONT HOTEL YA JIJINI MWANZA YAFUNGWA.

Hotel ya nyota tano ya JB Belmont iliyopo Jijini Mwanza imefungwa kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kushindwa kutimiza masharti ya mkataba kati yake na mmiliki wa jengo ilipo hotel hiyo Mfuko wa  Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Tangazo la kufungwa kwa hoteli hiyo lilitolewa juzi jumamosi asubuhi baada ya watumishi wa NSSF kubadika tangazo la kufungwa huduma katika hotel hiyo jambo lilichosababisha wateja waliokuwa wakifika hotelini hapo na kushangazwa na tangazo hilo.

Hata hivyo haikujulikana kama kulikuwa na wateja ndani ya hoteli hiyo kwa kuwa hakuna mtu aliyeruhusiwa  kuingia ndani ya hoteli hiyo ambapo eneo la mbele ya hoteli hiyo lilizungushiwa kamba kuashiria kwamba hakuna alieruhusiwa kuingia ndani.

Hoteli hiyo ambayo inamilikiwa na raia wa Uganda Justus Buguma (marehemu kwa sasa),  kabla ya kubadilishwa jina na kuitwa JB Belmont, ilikuwa ikijulikana kwa jina la Nyumbani Hoteli ikimilikiwa na aliyewahi kuwa  mbunge wa Jimbo la Vunjo (CCM), Aloyce Kimaro ambaye naye inadaiwa  kuwa aliondolewa na NSSF  ndani ya jengo hilo baada ya kushindwa kulipa kodi.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa  baada ya marehemu Bugumba kufariki dunia Februari 13, 2013 hoteli hiyo hivi sasa inamilikiwa na familia yake ambapo tena imekumbana na kisa kile kile kilichomkuta Kimaro.

Akizungumza kwa njia ya simu, Meneja wa NSSF Kanda ya Ziwa Hamis Fakhi alikiri hoteli hiyo kufungwa  huku akishindwa kubainisha sababu za kufungwa ambapo aliahidi kuzungumza na waandishi wa habari kesho.


“Ni kweli tumefunga hoteli hiyo lakini sina amelezo mengine zaidi ya hayo, kwani hata makubaliano ya mkataba kati ya mmiliki wa hoteli na NSSF yalifanyika makao makuu,” Amlisema Fakhi.

No comments:

Powered by Blogger.