LIVE STREAM ADS

Header Ads

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI ATEMBELEA MABANDA YA WIZARA YAKE KATIKA MAONYESHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA.

Afisa wa Jeshi la Magereza Nchini, Nsajigwa Mwankenja (kulia), akimpa maelezo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo yaNdani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil kuhusu huduma zinazotolewa na Jeshi hilo, alipotembelea banda la Wizara hiyo wakati wa maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
                                    Picha zote na Wizara ya Mambo yaNdani ya Nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo yaNdani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil, akiuliza swali mara baada ya kutembelea banda la Idara ya Uhamiaji wakati wa maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil, akisoma vipeperushi vya Idara ya Uhamiaji wakati alipotembelea Idara hiyo katika maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja,jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil, akiangalia zao la muhogo linalolimwa na Jeshi la Magereza mara baada ya kutembelea banda la Jeshi hilo wakati wa maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja,jijini Dar es Salaam. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil, akiweka saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), wakati wa maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ya nayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
Afisa Habari Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Rose Mdami (kulia) akimuelekeza Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bima nchini (TIRA),Israel Kamuzora, kujaza fomu ya kuomba kitambulisho cha Taifa wakati wa maonyesho ya Wiki yaUtumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.

No comments:

Powered by Blogger.