CHAMA CHA ACT WAZALENDO CHAJINADI KUIONDOA CCM MADARAKANI.
Na: Elisa Anatory
email: anatoryelisa@gmail.com
Contact: 0763 34 50 64.
Katibu wa chama cha Alliance For Change and Transparency ACT
Wazalendo Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Iddi Kiula amesema kuwa chama hicho
kimejipanga kushika nyazifa mbalimbali za Uongozi katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka
huu.
Kiula
aliyasema hayo jana ofsini kwake wakati
akizungumza na Binagi Media Group juu ya mikakati ya chama hicho katika kuelekea
kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu unaotarajiwa kufanyika Octoba 25.
Alisema kuwa chama hicho ambacho tangu
kuanzishwa kwake kimekuwa kikivuna wanachama wa kutosha kila kukicha katika
Wilaya ya Nyamagana, Mkoa wa Mwanza na Taifa kwa ujumla, kimenuwia kukiondoa madarakani
Chama cha Mapinduzi CCM kuanzia ngazi ya Udiwani, Ubunge pamoja na Urais.
"Wale wenye sifa za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi, fomu zinatarajiwa kuanza kutolewa kuanzia Julai Mosi hadi Julai 17
mwaka huu na gharama
za uchukuaji fomu hizo ni Shilingi Elfu Kumi kwa ngazi ya Udiwani, Elfu Ishirini kwa
Ubunge na Shilingi Laki Moja kwa nafasi ya Urais" Alisema Kiula.
Kiula alitanabaisha kwamba lengo la
kuweka kiwango hicho ambacho kinaonekana ni kidogo ukilinganisha na vyama
vingine kama CCM ambayo Fomu ya Urais ni shilingi Milioni Moja ni kutoa fursa kwa
yeyote mwenye uwezo wa kuwa kiongozi kupata nafasi ya kugombea.
Akihitimisha mazungumzo na Binagi
Media Group, Kiula aliwahimiza makada wa ACT Wazalendo wenye sifa za kugombea
nafasi mbalimbali za uongozi kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za kugombea
ambapo aliwahakikishia kwamba anaamini chama hicho kitaibuka na ushindi
mnono katika uchaguzi wa Mkuu wa Mwaka huu kutokana na sera zake imara ambazo zinakubaliwa
na Watanzania walio wengi.
No comments: