LIVE STREAM ADS

Header Ads

VICHAPO VYATAWALA KATIKA MASHINDANO YA KITAIFA YA UMITASHUMITA JIJINI MWANZA.

Na:Oscar Mihayo
Mashindano ya UMITASHUMITA yanayoshirikisha Shule za Msingi hapa nchini katika ngazi ya Kitaifa yamezidi kushika kasi katika viwanja vya Butimba Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza ambapo jana katika Mpira wa miguu wavulana Kilimanjaro wamewatungua mabao 4-3 wenzao wa Kagera Sugar.

Wafungaji katika Mchezo huo walikuwa ni Abraham Japhet, Rajabu Omary na Lameck Gudluck aliyefunga mawili, huku goli la Kagera likifungwa na Elick Edison, Fladius Tobias na Princepius Charles.

Na kwa upande wa  mpira wa wavu kwa wavulana  Timu ya Geita iliishinda Timu Rukwa kwa seti 2-0, Kigoma ikaichapa Tanga seti 2-0 na kwa wasichana Simiyu ikaichabanga Singida seti 2-0, Mtwara ikashinda seti 2-0 dhidi yaTanga na Pwani ikaibuka na ushindi wa seti 2-0 dhidi ya Shinyanga.

Na kwa mpira wa mikono Timu ya wavulana Lindi iliichapa Pwani mabao 22-4, Manyara ikaichapa Njombe mabao 11-5, Mwanza ikaicharaza Katavi mabao 11-5, na kwa wasichana Tabora ikainyuka Simiyu mabao 13-11, Mbeya ikaichapa Singida mabao 13-4 na Katavi ikashinda mabao 9-8 dhidi ya Tanga.

Mchezo mwingine wa mpira wa wavu kwa wavulana Mtwara iliichapa Kagera seti 2-0, Katavi ikashinda seti 2-0 dhidi ya Ruvuma,na Simiyu ikaicharaza Shinyanga seti 2-0.


Bado mashindano hayo yanaendelea Katika viwanja vya  Chuo Cha walimu Butimba ambapo yanatarajia kufikia tamati Julai tatu mwaka huu.

No comments:

Powered by Blogger.