LIVE STREAM ADS

Header Ads

BAADA YA ZIARA YA KIMASOMO BUNGENI, MENEJA WA FURAHA ENGLISH MEDIUM SCHOOL AZUNGUMZA.

picha haihusiani na habari
Na:Neema Joseph
WAMILIKI WA  SHULE  BINAFSI  NCHINI WAMESHAURIWA  KUZINGATIA  KUTOA ELIMU KWA VITENDO KATIKA SHULE ZAO ILI KUWAJENGEA   UWEZO WANAFUNZI JUU YA YALE WANAYOJIFUNZA DARASANI JAMBO LITAKALOSAIDIA KUINUA KIWANGO CHA ELIMU NCHINI.

HAYO  YALIBAINISHWA WIKI HII NA  MENEJA  WA  SHULE  YA  KIINGEREZA  YA  FURAHA   ENGLISH  MEDIUM  ILIYOKO   WILAYA  YA  NYAMAGANA   JIJINI MWANZA  JOAN  GOMBO  BAADA  YA  KUFANYA  ZIARA  BUNGENI  MJINI DODOMA.

GOMBO ALIBAINISHA  KUWA ELIMU  KWA  NJIA  YA  VITENDO  INASAIDIA    KUKUZA  UELEWA  KWA WANAFUNZI,  KWA KUWA  WANAJIFUNZA HUPATA FURSA YA KUJIFUNZA KWA  KUONA   VITENDO  VYA  SHUGHULI  HUSIKA.

NAYE  MWALIMU  MKUU WA  SHULE  HIYO  MWALIMU EMMANUEL  MANONI  ALISEMA  KUWA  SHULE YAKE ILIFANYA ZIARA BUNGENI KWA LENGO  LA KUBORESHA  ELIMU  KWA  VITENDO  KWA WANAFUNZI HUSUSANI KUFAHAMU  KAZI  ZA  MUHIMILI WA  BUNGE  KWA  KUWA  KAZI  ZA MUHIMILI  HUO  ZIPO  KWENYE  SILABASI  ZA MASOMO YA KUFUNDISHIA.

KWA  UPANDE WAO WANAFUNZI  WA SHULE  HIYO  RICHARD  EDWIN  PAMOJA NA   FAUZIA  STEVEN  WALIWAHIMIZA  WAZAZI  KUWA  NA  TABIA  YA  KUCHANGIA    ZIARA  ZA  MAFUNZO KWA VITENDO  KATIKA SHULE   WANAZOSOMA WATOTO WAO  KWA KUWA  ZINASAIDIA   KUKUZA  UELEWA  KWA WANAFUNZI KIVITENDO.

SHULE  YA   FURAHA   ENGLISH  MEDIUM ILITEMBELEA   BUNGE  LA  JAMHURI WA MUUNGANO WA TANZANIA  MWANZONI  MWA  WIKI HII  ILI KUWAPA  WANAFUNZI  NAFASI  YA  KUJIFUNZA  KAZI  ZINAZOFANYWA  NA  BUNGE HILO AMBALO NI MUHIMILI WA SERIKALI  ILI KUSADIFU   MAUDHUI  YANAYOFUNDISHWA  KWENYE   SILABASI   ZA MASOMO YAO.

No comments:

Powered by Blogger.