LIVE STREAM ADS

Header Ads

TIMU YA SOKA YA BUSWELU VETERANI YA ILEMELA KUKIPIGA NA UKEREWE VETERANI.

picha kutoka Maktaba
Na:Oscar Mihayo
Timu ya Soka ya Buswelu Veterani iliyopo Ilemela Mkoani Mwanza inatarajia kufanya ziara ya mchezo wa kirafiki katika Wilaya ya Ukerewe ambapo itanyukana na Ukerewe Veterani katika mchezo utakaofanyika Mjini Nansio.

Akizungumza na Binagi Media Group juzi, Mratibu wa ziara hiyo David Mpemba alisema kuwa ziara hiyo inatarajiwa kufanyika Juni 27 hadi 28 mwaka huu.

Mratibu huyo aliongeza kuwa lengo kubwa la mchezo huo ni kudumisha mahusianao kati ya wachezaji wakongwe wa Wilaya za Ilemela na Ukerewe pamoja na kujenga udugu wa kikabila kati ya wakerewe na wasukuma.

Timu hiyo inatarajia kuambatana na viongozi Richard Chizi ambae ni Mwenyekiti, George Simon ambae ni Katibu, Alex Simon ambae ni Mweka Hazina, Robert Julius mchunga ambae ni nidhamu Nidhamu, Martine Ruta ambae ni Mwanasheria,Deus Pole ambae ni Meneja, Silvery Mukai ambae ni Kocha, Hoja Lukuba ambae ni Nahodha na Gibson ambae ni Kaptani Msaidizi.

Aidha wachezaji timu ya Buswelu ni pomoja na  Enock Bundala, Lucas Bundala, James Costantine, Edwin Kaaya, Willison Jangwani, Osward Mbonde, Sunday Mussa, Hubert Matau, Maarufu  Vodacomn. Silvester Amiri, Manisha Ngeze, Juma Masule, Mrisho Masebu, Andrew Vedastus, Peter Onyango na Mohamed Steker.

Nayo Timu ya Ukerewe Veterani inatarajiwa kuongozwa na baadhi ya wachezaji wastaafu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kama Moshi Kazimoto ambae amewahi kuichezea timu ya Simba na Juma Maka ambae amewahi kukipiga na timu ya Pamba ambao wanatajia kuonyesha makeke yao ya enzi hizo.

Mchezo kati ya Timu hizo unatarajiwa kupigwa katika Uwanja wa Getruda Mongela uliopo Mjini Nansio, Ukerewe.

No comments:

Powered by Blogger.