LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KATIKA SIKU YA KUPIGA VITA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA.

Katikati ni Edwin Soko ambae ni Mwenyekiti wa OJADACT akitoa taarifa kwa Vyombo vya Habari hii leo juu ya Maadhimisho ya Siku ya Kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya Duniani yanayotarajiwa kufanyika Kesho. Kulia ni Neema Joseph ambae ni Mhasibu wa OJADACT na Kushoto ni Isaack Wakuganda ambae ni Afisa Jinsi OJADACT. 
Chama  cha  waandishi wa habari wa kupiga  vita  matumizi  ya  dawa  za kulevya  na uhalifu Tanzania (ojadact)  leo  tunafanya  mkutano na nyinyi    ikiwa  maudhui  makubwa ni   kampeni  zetu kuelekea  kwenye  maadhimisho ya  kidunia  ya  kupiga vita   matumizi  ya  dawa za kulevya  duniani, juni 26, 2015.

Ndugu  waandishi wa  habari  maadhimisho  ya  mwaka  huu kitaifa  yatafanyika   mkoani pwani  wilaya  ya bagamoyo, na kimkoa  yatafanyika   eneo  la  igogo . Kauli  mbiu    ya  mwaka  huu  itakuwa  ni, jenga  jamii, maisha   na  utu  bila  dawa za kulevya.

Hali  ya  dawa za kulevya   kitaifa:
Ndugu  waandishi  licha  ya   kuadhimisha  kila  mwaka  siku  ya  kupiga  vita   matumizi    ya  dawa za kulevya  duniani  tatizo  la  dawa  za   kulevya limeendelea  kuwa  kubwa kiasi  cha  kutia  shaka, tuna  imani   juhudi  kubwa  zinahitajika  za  kupambana  na  dawa za kulevya.

Kitakwimu   ripoti mpya ya ofisi ya umoja wa mataifa ya kupambana na mihadarati na uhalifu (unodc), imesema tanzania ni kinara wa kupitisha dawa za kulevya katika nchi za afrika mashariki. Ripoti hiyo, imesema jumla ya tani 64 za dawa za kulevya aina ya heroine, zilisafirishwa bila kukamatwa kwenda au kupitia afrika mashariki, ikiwemo tanzania kati ya mwaka 2010 na 2013.

Ripoti hiyo, imesema nchini tanzania mji wa tanga, ndio kinara na njia kuu ya kusafirishia dawa hizo kwani tangu mwaka 2010, ukamataji uliongezeka kutoka kilo 145 hadi kilo 813 mwaka huu.

Wastani wa ukamataji wa shehena za dawa za kulevya eneo hilo, uko katika kilogramu 1,011 mwaka 2013 kutoka 145 kilo za awali.

Takwimu zinaonyesha kwa pamoja watanzania na wakenya, wanaongoza kwa utumiaji na usafirishaji dawa za kulevya aina ya cocaine, huku wakitumia dola milioni 160 kila mwaka. Lakini katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, kati ya mwaka 2010 na 2013, shehena zilizokamatwa na maofisa husika nchini tanzania, kenya, shelisheli  na  mauritius zilikuwa tani 1.6

Hali  ya   matumizi  ya  dawa za kulevya  Mkoa wa Mwanza.
Mkoa wa Mwanza unakadiliwa  kuwa na watumiaji  wa dawa za kulevya wapatao 10,000  kwa mujibu wa takwimu  za mganga  mkuu wa mkoa wa mwanza.

Kwa  mujibu wa  tafiti   ya tume  iliyofanywa  Mwanza, wilaya  ya  nyamagana  na ilemela   hadi  kufikia  agosti, 2014  ilikuwa na  watumiaji  wa dawa za kulevya  wapatao 3,300, kati  yao  wanaojidunga   walikuwa 300.

Pia kwa mujibu wa  shirika  la  icap  hadi  kufikia   mei, 2015  watumiaji wa dawa 1093  walijitokeza  kupima   ukimwi  ili kujua  afya  zao.

Mtazamo  wa Chama(OJADACT)
Licha  ya  tatizo  la dawa  za kulevya  kuendelea  kuwa   kubwa, hakuna  jitihada  za  dhati  zinazolingana  na  ukubwa wa tatizo  zilizoonyeshwa  na  serikali  pamoja  na  Taifa  kwa  ujumla  ili  kukabiliana  na  hali iliyopo. 

Kumekuwa  na   uzembe  wa makusudi wa  kutaja  nafasi  ya  Nchi  kimataifa   juu  ya  tatizo  la  dawa  za kulevya  na badala  yake   serikali imekuwa  ikificha  uhalisia  wa tatizo. 

Tafiti  na ripoti za kimataifa  ndizo  pekee  zimekuwa  zikionyesha  ukweli  juu  ya  tatizo  la dawa  za kulevya  kimataifa.

Rai  yetu  kwa  Nchi
•Vita   dhidi  ya  dawa  za kulevya  zinahitaji  nguvu  za pamoja ili  kukomesha biashara  hiyo
•Serikali na  taasisi  mbalimbali  zijikite  katika  kutoa  elimu  ya  kutosha  juu  ya  dawa za kulevya.
•Upatikanaji  wa  sera  ya  dawa  za kulevya  uharakishe  ili  kusaidia  kumaliza  tatizo
•Sheria  mpya  ya  dawa za kulevya  ya  mwaka 2014 isimamiwe  na kutekelezwa  ili kuleta  tija kwa Taifa
•Vita  dhidi  ya  dawa za kulevya  zitangazwe  kuwa janga  la kitaifa
•Moja  ya  sifa  za Rais  ajaye    iwe ni kuwa  na  uwezo wa kukabiliana  na  biashara  ya  dawa za kulevya  kama  alivyofanya  Rais  Richard  Nickson  wa Marekani
•Serikali  iweke  wazi ukubwa wa tatizo  la  dawa za kulevya  ili  Taifa  liweze kujitathimini  na kutafuta  njia  mbadala  ya  kumaliza  tatizo.

Ushiriki wa  maadhimisho 
Ndugu waandishi wa habari  maadhimisho  ya  mwaka  huu  kitaifa  yatafanyika  Mkoa wa Pwani , wilaya ya  Bagamoyo, ambako  OJADACT tutashiriki  na kimkoa   yatafanyika   kata  ya  Igogo, hivyo  basi  tunawaomba  waandishi  wote  kushiriki kikamilifu  kwenye  maadhimisho  hayo  yenye  kauli mbiu, JENGA  JAMII, MAISHA  NA  UTU BILA DAWA ZA KULEVYA.

Salamu  toka kwa  Katibu  Mkuu wa  Umoja wa mataifa.
Kila  mtu ajitathimini   kuwa  ametimiza   jukumu  lake  la kuilinda  jamii   dhidi  ya  janga  la dawa za  kulevya.
Nawashukuru sana  ndugu waandishi  wa habari.
Edwin   soko
Mwenyekiti
OJADACT.
Neema Joseph (Kulia) ambae ni Mhasibu wa OJADACT akitoa ufafanuzi juu ya Maadhimisho ya Kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya yanayotarajiwa kufanyika Kesho. Kushoto ni Edwin Soko ambae ni Mwenyekiti wa OJADACT.
Wanahabari Mkoani Mwanza
Wanahabari Mwanza

No comments:

Powered by Blogger.