LIVE STREAM ADS

Header Ads

KAMANI ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA URAIS. AAHIDI KUFUFUA VIWANDA VILIVYOKUFA NCHINI.

Harakati za Wanasiasa mbalimbali ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM kutangaza nia ya Kugombea nafasi ya URAIS nchini zinaendelea kwa kasi ya ajabu huku zikiwa na mbwembwe ambazo hazijawahi kuonekana katika awamu zote nne zilizopita. Baada ya harakazi hizo za kutangaza nia ya kugombea urais ndani ya CCM kufunguliwa na Mbunge wa Jimbo la Monduli Mkoani Arusha na Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward Ngoyai Lowassa (CCM) siku ya Jumamosi ya May 30, 2015, Wengi wamejitokeza na kutangaza nia.
Na:George GB Pazzo
Hii leo Binagi Media Group inakuletea kilichojili jana June 02, 2015 wakati Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mh.Titus Kamani (Pichani juu) ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Busega Mkoani Simiyu akitangaza nia ya Kugombea Urais kupitia tiketi ya CCM katika Ukumbi wa "Gand Hall" Jijini Mwanza.

Pamoja na mambo mengine, Mh.Kamani alibainisha kwamba akipata fursa ya kuwa Rais wa Tanzania, atahakikisha kuwa anafufua viwanda vilivyokufa nchini lengo likiwa ni kusaidia katika kuinua thamani ya mazao ya wakulima na wafugaji kupitia viwanda hivyo pamoja na kuimalisha ajira binafsi kwa watanzania.

Alisema atahakikisha anaboresha mageuzi katika Kilimo nchini kwa kilimo ndiyo sekta pekee inayoweza kuondoa umaskini nchini huku pia akibainisha kuwa atahakikisha anafanya mageuzi makubwa katika Sekita ya Madini, Elimu, Afya na nyinginezo ili kuhakikisha Tanzania inasonga mbele kimaendeleo.
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mh.Titus Kamani ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Busega Mkoani Simiyu akitangaza nia ya Kugombea Urais kupitia tiketi ya CCM katika Ukumbi wa "Gand Hall" Jijini Mwanza. 
Mh.John Lembeli ambae ni Mbunge wa Jimbo la Kahama Mkoani Shinganya (CCM) akisoma Wasifu wa Mh.Kamani.
Meza Kuu
Viongozi wa Dini
Wananchi  na Makada wa CCM wakifuatilia hotuba ya Mh.Kamani wakati akitangaza nia ya kugombea Urais kwa tiketi ya CCM Jijini Mwanza
Wanahabari nao walikuwepo pia
Umati wa watu ukifuatilia hotuba ya Mh.Kamani katika Ukumbi wa "Gand Hall" wakati akitangaza kugomea Urais jana.
"Tulinde Rasilimali Zetu"
Ukumbi ulilipuka baada ya Mh.Kamani kutangaza nia ya Kugombe Urais katika Uchaguzi wa Mwaka huu unaotarajiwa kufanyika Mwezi Octoba.

No comments:

Powered by Blogger.