LIVE STREAM ADS

Header Ads

OPARESHENI FUNGASHA VIRAGO WENJE JIMBO LA NYAMAGANA YAFICHUA MADUDU YA MAKUBWA.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoani Mwanza Miraji Mtaturu akihutubia katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika jana jumamosi May 30, 2015 katika Uwanja wa Mirongo Jijini Mwanza. Mkutano huo pia ulitumika kumtambulisha John Lipesi Kayombo (hayupo pichani) ambae ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) akiwakilisha Vyuo Vikuu hapa nchini.
 Na:BINAGI MEDIA GROUP
Siku chache baada ya kutuhumiwa kutumia fedha za mfuko wa jimbo vibaya, Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza Ezekiel Wenje (Chadema) ameingia tena katika Kashfa nyingine, baada ya kuelezwa  kuwa ametafuna mamilioni ya pesa kupitia taasisi yake.

Hayo yalielezwa jumamosi iliyopita ya May 30, 2015 na Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoani Mwanza Miraji Mtaturu, wakati akiwahutubia wananchi katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Mbugani Jijini Mwanza.

Katika Mkutano huo Mtaturu alianza kwa kuwakumbusha wananyamagana juu ya mbunge wao kutumia zaidi ya Shilingi Milioni 40 kwa matumizi yasiyo sahihi ambayo  ni pamoja na kulipana posho katika kipindi alichoingia madarakani, tuhuma ambazo hata hivyo Wenje alizikana hivi karibuni wakati akiwahutubia wapiga kura wake katika Uwanja huo huo wa Mbugani.

Kuhusu tuhuma za kutafuna pesa, Mtaturu alibainsha kwamba Mwaka 2012 Wenje aliitisha harambee kwa ajili ya kuwasaidia vijana wanaoishi katika Mazingira magumu kupata elimu kupitia taasisi yake ya Nyamagana Education Foundation lakini pesa zilizopatikana katika harambee hiyo hazikutumika kama ilivyokusudiwa.

"Katika harambee hiyo zaidi ya Shilingi bilioni 75 ziliweza kupatikana lakini jambo la kusikitisha ni kwamba Wenje alitimkia Dar es salaam baada ya harambee hiyo, je hapo mna mbunge kweli?" Alihoji Mtaturu huku akiongeza kuwa miongoni mwa taasisi ambazo ziko katika orodha ya kufutiwa usajili na Wizara ya Mambo ya Ndani ni pamoja na Taasisi ya Mh.Wenje ambayo alisema pia ndani yake imesheheni ndugu zake akiwemo raia wa Kenya jambo ambalo ni kinyume cha Katiba ya nchi.

"Tunataka kabla taasisi hiyo haijafutiwa usajili, Wenje aje hapa awaambie zilipo pesa alizochangisha katika harambee ya taasisi yake".Alisema Mtaturu ambae alibainisha kuwa Oparesheni Fungasha Virago Wenje katika jimbo la Nyamagana imeanza rasmi hivyo Wenje ajiandae kuachia jimbo hilo.

Juhudi za Binagi Media Group Kumpata Mh.Wenje ili kuzungumzia tuhuma hizo bado hazijazaa matunda hivyo endelea kuwa pamoja nasi ili kujua atakachokizungumza pindi atakapopatikana.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza wakati akiwasili katika Uwanja wa Mirongo Jijini Mwanza jana kwa ajili ya kuwahutubia wanaccm pamoja na wananchi.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtatururu (wa pili kushoto) akipokea kadi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA waliojiunga na CCM siku ya jana.
Mmmoja wa Vijana wa CHADEMA (Mwenye kinasa sauti) akizungumza kwa niaba ya wenzie waliojiunga na CCM jana katika Uwanja wa Mirongo Jijini Mwanza.
John Lipesi Kayombo ambae ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) anaewakilisha Vyuo Vikuu nchini akizungumza jana katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Mirongo Jijini Mwanza.
John Lipesi Kayombo ambae ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) anaewakilisha Vyuo Vikuu nchini akizungumza jana katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Mirongo Jijini Mwanza.
Katibu wa Itikadi na Uenezi Mkoa wa Mwanza Simon Mangelepa akizungumza katika Mkutano wa CCM uliofanyika jana katika Uwanja wa Mirongo Jijini Mwanza.
Kutoka kushoto ni Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana Elias Mpanda, akifuatiwa na Mwenyekiti wa Vijana CCM Wilaya ya Nyamagana Hussein Kim (Katikati) pamoja na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilemela Henry James
Gerald Josephat aliekuwa Mwenyekiti wa Chadema Kata ya Terrat Arusha Mjini (Mwenye kinasa sauti) akiwa pamoja na Revocatus Parapara (nyuma ya jukwaa) aliekuwa Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha kwa miaka 16, Mjumbe Mkutano Mkuu Chadema Taifa, Mjumbe wa Baraza la Mashauriano Mkoa wa Arusha ambae alichomoka Chadema tangu mwezi wa tatu mwaka jana.
Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana Elias Mpanda
Viongozi wa CCM Mkoani Mwanza
Viongozi wa CCM Mkoani Mwanza
Burudani pia ilikuwepo
Wananchi na WanaCCM wakifuatilia Mkutano wa CCM uliofanyika jana katika Uwanja wa Mirongo Jijini Mwanza.
Hizi ndizo jumbe kutoka Kwa Vijana

No comments:

Powered by Blogger.