LIVE STREAM ADS

Header Ads

MICHUANO YA UMITASHUMITA NGAZI YA TAIFA YAFIKIA PATAMU. HAKIKA MTOTO HATUMWI DUKANI.

Na:Oscar Mihayo
Hatua ya mtoano ya michuano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi Tanzania UMITASHUMITA ngazi ya Taifa yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Chuo cha Ualimu Butimba Jijini Mwanza imeendelea kupamba moto ambapo timu ya soka ya wavulana  kutoka Mkoani Shinyanga imeitundika bao 1 -0 timu ya Kagera Sugar kutoka Mkoani Kagera.

Mfungaji wa bao la Shinyanga katika mpambano huo uliochezwa juzi alikuwa ni Juma Miraji.

Michezo mingine ilikuwa ni kati ya Manyara ambapo Manyara iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Dodoma huku Mara ikiinyuka bao 3-0 timu ya Rukwa.

Kwa upande wa Mpira wa Netball Mara iliibuka na Seti 23 dhidi ya Seti 12 za Singida, Mbeya iliibuka na Ushindi wa Seti 31 dhi ya dhidi ya Seti 9 walizopata Iringa, Katavi iliibuka na Ushindi wa Seti 23 dhi ya Seti 22 za Mtwara huku Rukwa ikiibuka na Ushindi wa Seti 2 dhidi ya Kigoma iliyoambulia patupu.

Matokeo mengine ya mpira wa mikono wa wavulana Mbeya seti 13 dhidi ya Simiyu seti 7, Rukwa seti 15 dhidi ya Tanga seti 15, Tabora seti 7 dhidi ya Arusha seti 15, Dar es Salaam seti 27 dhidi ya Kagera seti 3, Kilimanjaro seti 12 dhidi ya Singida seti 8.

Kwa upande wa wasichana Mpira wa Mikono Mtwara ilipata Seti 5 dhidi ya Morogoro Seti 8, Simiyu Seti 10 dhidi ya Kigoma Seti 7. 

Mashindano hayo yanaendelea katika viwanja hivyo na wiki hii yameingia katika nafasi ya robo fainali ambapo yanatarajiwa kufikia tamati Julai tatu mwaka huu.

No comments:

Powered by Blogger.