LIVE STREAM ADS

Header Ads

KONISAGA ATOA RAI KWA EWURA. NI KATIKA UZINDUZI OFISI ZAKE KANDA YA ZIWA.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga (Mtumishi wa Mungu).
Na:George GB Pazzo
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini UWURA imetakiwa Kusimamia Sekta za Nishati na Maji kwa njia ya Uwazi na haki kwa lengo la kuzalisha tisha kwa watumiaji wake.

Hayo yalisemwa wiki iliyopita na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Baraka Konisaga, wakati akifunguzi wa Ofisi ya Mamlaka hiyo Kanda ya Ziwa iliyopo Jijini Mwanza.

Konisaga alisema kuwa Mamlaka ya EWURA ambayo ni Mdhibiti wa huduma za Nishati na Maji, inapaswa kusimamia vyema huduma zake kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizopo kwa lengo la kuleta usawa na kuongeza tija na kuleta unafuu wa matumizi baina ya pande mbili zinazohusika ambazo ni muuzaji na mtumiaji wa nishati hizo.

Aidha Konisaga amesema kuwa Serikali itaendelea kuandaa sera madhubuti ili kusimamia Nishati ya Udhibiti wa Nishati na Maji ikiwa ni pamoja na kujenga miundombinu ambayo itawavutia wawekezaji katika sekta hizo ili kuleta unafuu kwa wananchi.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi EWURA Simon Sayore ametoa wito kwa Wafanyabiashara na Watoa huduma za Nishati na Maji kuhakikisha kuwa wanaboresha huduma wazitoazo ili kufikia kiwango kinachohitajika jambo litakalowasaidia kuondokana na hatari ya kufungiwa shughuli zao.


Nae Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Felix Ngamlagosi amesema kuwa mamlaka hiyo itaendelea kuboresha huduma zake kwa kutatua changamoto zinazoikabili ikiwa ni pamoja na kuendelea kufungua ofisi katika kanda mbalimbali hapa nchini kwa ajili ya kufikisha huduma karibu na wananchi.

EWURA imefungua ofisi yake ya Kanda ya Ziwa Jijini Mwanza ikiwa ni Mkakati wake wa Kufungua Ofisi za Kanda kote nchini ambazo ni Kanda ya Kanda ya Kaskazini itakayokuwa Mkoani Arusha, Kanda za juu Kusini Mkoani Mbeya, Kanda ya Kati Mkoani Dodoma, Kanda ya Maghari Mkoani Kigoma pamoja na Kanda ya Kusini itakayokuwa Mkoani Mtwara.

No comments:

Powered by Blogger.