LIVE STREAM ADS

Header Ads

MSTAHIKI MEYA WA JIJI LA MWANZA STANSLAUS MABULA AIFAGILIA KAMPUNI YA SOLAR YA MOBISOL.

Katikati ni Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza ambae pia ni diwani wa Kata ya Mkolani (CCM) Stanslaus Mabula akipokea Moja ya aina ya Mtambo wa Uzalishaji Umeme wa Jua ambao uliahidiwa kutolewa na Kampuni ya Uuzaji wa Mitambo ya Kufua Umeme wa Jua ya MOBISOL kwa ajili ya kupelekwa katika maeneo yenye uhitaji wa Umeme kama vile Vituo vya Zahanati Jijini Mwanza. 
Na:George GB Pazzo
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula ameipongeza Kampuni ya Mobisol ambayo inajihusisha na Uuzaji na Ufungaji wa Mitambo ya kufua umeme wa Jua kutokana na utoaji wa huduma bora katika jamii.

Mabula alitoa kauli hiyo wiki iliyopita alipotembelea Makao Makuu ya Kampuni hiyo yaliyopo Kisesa Wilayani Magu, kwa lengo la kujionea utendaji kazi wa Kampuni hiyo.

Alisema kuwa bado asilimia kubwa ya Watanzania hawapati huduma ya Umeme wa Tanesco hivyo ujio wa Kampuni hiyo ya Mobisol umeleta unafuu kwa Watanzania ambao bado hawajafikiwa na huduma ya Umeme.

"Watanzania zaidi ya asilimia 70 bado hawapati huduma ya Umeme hivyo ujio wenu ni nafuu hasa kwa wananchi wa kawaida maana wanapunguza matumizi ya vibatari na kwa kuwa huu ni mwanzo naamini kwamba hata suala la gharama mtaliangalia ili iwepo gharama nafuu zaidi itakayoruhusu kila mwananchi kupata mfumo wa umeme wa solar za Mobisol" kwa gharama nafuu zaidi. Alisema Mabula.


Akitoa ufafanuzi juu ya Utendaji kazi wa Kampuni ya Mobsol, Albert Msengezi ambae ni Meneja Masoko wa Kampuni hiyo Kanda ya Ziwa aliahidi kuwa Kampuni yake itatoa Mitambo kadhaa ya kufua Umeme wa Jua kwa ajili ya kusaidia upatikanaji wa Nishati ya Umeme katika zahanati mbalimbali Jijini Mwanza ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya.

No comments:

Powered by Blogger.