MABULA 2015 INAWEZEKANA JIMBO LA NYAMAGANA MKOANI MWANZA. ASEMA MPANGO UPO WAZI.
Diwani wa Kata ya Mkolani (CCM) Stanslaus Mabula ambae pia ni Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza.
Binagi Media Group
Diwani wa Kata ya Mkolani Jijini Mwanza (CCM) ambae pia ni Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula, amesema kuwa anao mpango wa Kujitosa katika kinyang'anyiro cha Uchaguzi wa Mwaka huu wa 2015. Mabula aliyasema hayo hivi karibuni wakati akizungumza na Binagi Radio ya Binagi Media Group juu ya tetesi zilizopo mitaani kwamba anao mpango wa kugombea ubunge katika jimbo la Nyamagana katika Uchaguzi wa Mwaka huu unaotarajajia kufanyika mwezi Octoba 25 mwaka huu.
"Mpango lazima utakuwepo hauwezi ukawa wakati wa uchaguzi halafu wewe mwanasiasa usiwe na mpango wa kugombea, utakuwa mwanasiasa wa ajabu sana hivyo wakati ukifika nitasema kama natetea nafasi yangu au ni nasonga mbele kwani lolote linawezekana". Alisema Mabula huku akishindwa kuainisha nafasi ya uongozi anayotarajia kugombea.
Huku akishindwa kuainisha ni lini mpango wake wa kuweka bayana nafasi ya uongozi anayotarajia kuigombea katika uchaguzi wa mwaka huu, Mabula alibainisha kuwa fomu kwa wagombea wa nafasi za udiwani na Ubunge kupitia chama cha Mapinduzi zinatarajiwa kuanza kutolelewa Julai 13 mwaka huu hivyo huo ndio utakuwa muda mwafaka wa yeye kuweka mambo hadharani.
Wakati Mabula akijikanyaga kuweka hadharani nafasi ya uongozi anayotarajia kuigombea mwaka huu, tayari kelele zimekwisha anza kusikika kuwa anao mpango wa kugombea nafasi ya Ubunge jimbo la Nyamagana kupitia CCM na kwamba uwezekano wa kulinyakua jimbo hilo kutoka mikononi mwa Hezekiel Wenje (CHADEMA) ni mkubwa kutokana na namna alivyowatumikia vyema wanamkolani na Jiji la Mwanza kwa ujumla katika kipindi chake cha Uongozi kinachoelekea ukingoni.
BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA BINAGI RADIO
No comments: