LIVE STREAM ADS

Header Ads

MSIMU WA PILI WA MTAA KWA MTAA YA METRO FM KUANZA TENA.

Na:George GB Pazzo
Kile Kipengere cha "MTAA KWA MTAA" kilichokuwa kikiruka hewani kupitia 99.4 Radio Metro Fm ya Jijini Mwanza, kimerejea tena hewani kwa kasi ya ajabu.

Kwa miezi kadhaa kipengere hicho hakikuwa hewani baada ya kumalizika kwa Msimu wa Kwanza wa Mtaa kwa Mtaa, msimu ambao ulionyesha mafanikio makubwa.

Kipengere hicho cha Mtaa kwa Mtaa huruka katika Kipindi cha Pambazuko la Metro Fm kinachoruka hewani Kila siku za Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 06:00 hadi saa 09:00 za asubuhi ikiwa ni miongoni mwa vipindi vingine.

Katika Kipengere hicho, masuala mbalimbali yanayoihusu jamii huzungumzwa na wanajamii (Wananchi) wenyewe huku yale yanayohitaji majibu kama vile changamoto za Kiafya, Elimu, Miundombinu, Kisiasa pamoja na mengine mengi hupatiwa majibu na mamlaka husika.


Katika Kipindi cha Kwanza cha Msimu wa Pili wa Kipengere hicho, wakazi wa Mabatini Jijini Mwanza watapata fursa ya kusikika ambapo Kesho Jumatano June 04, 2015 timu nzima ya 99.4 Radio Metro Fm itawatembelea wakazi hao kwa ajili ya maandalizi ya Mtaa kwa Mtaa Msimu wa Pili.

"Mtaa kwa Mtaa Msimu wa Pili tumejipanga upya na katika Msimu huu tutakuja kiutofauti kabisa maana tutaweza pia kukabiliana na baadhi ya changamoto ambazo tulikumbana nazo katika msimu wa kwanza, hivyo kwa kuanza tutaanza na wakazi wa Mabatini kama ilivyokuwa katika Msimu wa Kwanza ambapo tutazungumza nao LIVE hivyo wakazi wa Mitaa yote ya Mabatini kaeni tayari kwa ajili ya ujio wetu". Alisema hii leo Alphonce Tonny Kapela ambae ni Meneja Ubunifu Vipindi Radio Metro.

No comments:

Powered by Blogger.