LIVE STREAM ADS

Header Ads

DIWANI WA KATA YA KITANGIRI WILAYANI ILEMELA HENRY MATATA KUVUNJA UKIMYA JUMAMOSI HII.

Matata akiwahutubia wanakitangiri mwaka jana
Na:Georgr GB Pazzo
Diwani wa Kata ya Kitangiri Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza Henry Matata, anatarajia Kuwahutubia wananchi wa Kata hiyo katika Mkutano wa hadhara unaotarajiwa kufanyika Wikendi ijayo katika Viwanja vya Minazi Mitatu Kona ya Bwiru Wilayani humo.

Mkutano huo unatarajiwa kufanyika Jumamosi hii June 06, 2015 kuanzia saa nane mchana ambapo atakuwa Mwenyeji wa Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu ambae kama kawaida yake anatarajiwa kurindima katika Mkutano huo.

Masuala mbalimbali yanatarajiwa kuzungumzwa katika Mkutano huo ikiwa ni pamoja na Msimamo wa Matata ambae hivi karibuni alitangaza kuwania nafasi ya udiwani kwa awamu nyingine kwa tiketi ya CCM, baada ya kutimuliwa ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema mwaka 2012.

Lakini pia Matata anatarajia kutumia Mkutano huo kuwaeleza wanakitangiri mafanikio ya Kimaendeleo katika kipindi cha uongozi wake ambao unaelekea ukingoni, pamoja na baadhi ya changamoto ambazo amekumbana nazo katika uongozi wake na namna ya kukabiliana nazo.

Hakika huo si Mkutano wa Kukosa hivyo ni vyema wewe Mwananchi wa Kitangiri, Ilemela na Mkoa wa Mwanza kwa Ujumla ukahakikisha unafika katika Mkutano huo ili uweze kusikia nini ambacho kitazungumzwa ambapo pia utapata nafasi ya kuuliza maswali kwa wazungumzaji.
BONYENYA PLAY HAPA CHINI KUMSIKILIZA MATATA                              KUHUSU KUGOMBEA BONYEZA HAPA

No comments:

Powered by Blogger.