LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAKAZI WA MABATINI JIJINI MWANZA WASHAURIWA KUHAMA KABLA NYUMBA ZAO HAZIJABOMOLEWA.

GB Pazzo kutoka Radio Metro na Mmiliki wa Mtandao huu (Kulia) akifanya Mahojiano na Katibu wa CCM Kata ya Mbugani Gerald Mashalla (Kushoto).
Na:George GB Pazzo
Wakazi waishio maeneo ya kandokando ya mto Mirongo Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza, wameshauriwa kuhama katika maeneo hayo kwa lengo la kuondokana na uwezekano wa kubomolewa nyumba zao.

Katibu wa Chama cha Mpinduzi CCM kata ya Mbugani Gerald Mashalla alitoa uashauri huo hii leo wakati akizungumza na Radio Metro kupitia Kampeni yake ya Mtaa kwa Mtaa, Kata kwa Kata juu ya Mikakati ya Kata hiyo katika kupambana na mafuriko ambayo hutokea mara kwa mara katika eneo la Mabatini na hivyo kusababisha athari kubwa kwa wananchi.

Mashalla alibainisha kuwa CCM Kata ya Mbugani imeandaa mikakati ya kuwashirikisha wananchi wanaoishi kando kando ya Mtu huo ili waweze kuhama kwa hiari yao, kabla ya utekelezaji wa sheria ya kubomoa nyumba zao haijaanza kutekelezwa.

Alisema kuwa ujenzi holela wa nyumba kandokando ya Mto huo ndio umekuwa ukisababisha maji ya Mto Mirongo kushindwa kupita katika Mkondo wake na hivyo kusababisha mafuriko wakati wa masika.

Kutokana na sababu hiyo, Mashalla aliwasihi wananchi kuondoa makazi yao katika maeneo yanayozunguka mto huo, kabla taratibu za Kuwaondoa kisheria hazijaanza kutekelezwa ambapo nyumba zao zitabomolewa.


Baadhi ya Wananchi Mtaa wa Mabatini walieleza kuwa Serikali inapaswa kuwatafutia maeneo mbadala kwa ajili ya makazi yao, kabla ya uamuzi wa makazi yao kubomolewa huku wakiitupia lawama kutokana na kushindwa kuwazuia tangu awali wakati nyumba hizo zikijengwa.
Timu ya Radio Metro Fm ikiwa katika Ofisi za CCM Kata ya Mbugani Jini Mwanza Jana ambapo kutoka Kushoto ni Julieth Kashaigili, Jay Joh pamoja na Alphonce Tonny Kapela ambapo wa Kwanza Kutoka Kulia ni Rashid Rwango ambae ni Katibu wa Wazazi Kata ya Mbugani (CCM) na Wa pili Kulia ni Katibu wa CCM Kata ya Mbugani Gerald Mashalla.
Credit:Radio Metro Fm

No comments:

Powered by Blogger.