LIVE STREAM ADS

Header Ads

ZAIDI YA WAENDESHA BODABODA 200 WAUAWA MKOANI MWANZA HUKU BODABODA ZAIDI YA 3,000 ZIKIPORWA.

Na:George GB Pazzo
Waendesha Pikipiki maarufu kwa Jina la bodaboda zaidi ya 200 wameuawawa Mkoani Mwanza kutokana na matukio ya kuvamiwa na kutekwa huku pikipiki zaidi ya 3,000 zikiibiwa.

Hayo yalielezwa wiki iliyopita na Katibu wa Umoja wa Waendesha Pikipiki Mkoa wa Mwanza Abubakary Hussein, alipokuwa akizungumza na Mtaa kwa Mtaa ya Radio Metro Fm katika Ofisi za Umoja huo zilizopo Kata ya Mbugani Jijini Mwanza.

Hussein alisema kuwa idadi hiyo ni kwa kipindi cha kuanzia Mwaka 2011 hadi mwa mwaka huu, idadi ambayo amebainisha kuwa inawatia hofu kubwa waendesha pikipiki katika shughuli zao.

Hussein alibainisha kuwa asilimia kuwa matukio hayo hutokea kwa Waendesha pikipiki kukodishwa na baadhi ya waharifu ambao hujifanya ni abiria na kisha kuwateka na kuwapora pikipiki jambo ambalo wakati mwingine husababisha umauti kwa waendesha pikipiki.

Katika hatua nyingine Hussein aliziomba halmashauri za Mkoa wa Mwanza ikiwemo Hamashauri ya Jiji la Mwanza kuainisha vituo vya Waendesha pikipiki kwa lengo la kusaidia kuwatambua waendesha pikipiki.

Makamu Mwenyekiti wa Umoja huo wa Waendesha Pikipiki Mkoa wa Mwanza Seif Mussa Kagoma alibainisha kuwa kwa muda mrefu wamekuwa na juhudi za kutaka kuubaini mtandao wa Wezi wa Pikipiki Mkoani Mwanza, lakini juhudi hizo zimekuwa zikikwamishwa na baadhi ya polisi ambao wamekuwa wakirudisha nyumba jitihada za kubaini mtandao huo.

Alisema kuna mtuhumiwa wa wizi wa pikipiki aliwahi kukamatwa Mkoani Mwanza na akaahidi kuwataja wenzake baada ya kufikishwa katika kituo cha Polisi, lakini mtuhumiwa huo ilielezwa kuwa alifikishwa Mahakamani kabla hata hajawataja wenzake jambo ambalo linakwamisha kuubaini Mtandao wa wezi wa Pikipiki Mkoani Mwanza.

Juhudi za kupata idadi ya Waendesha Bodaboda waliouawa na Bodaboda zilizoporwa katika kipindi cha mwaka 2011/15 pamoja na juhudi za kukabiliana na matukio hayo kutoka jeshi la polisi Mkoani Mwanza bado zinaendelea.
                                     Credit.Radio Metro

No comments:

Powered by Blogger.